44
Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya mwana wa Korah.....
1 Mungu, tumesikia kwa masikio yetu, baba zetu wametuambia kazi uliyofanya katika siku zao, siku za kale.
2 Uliwafukuza mataifa kwa mkono wako, lakini ukawafanya watu wetu kuishi humo; wewe uliwataabisha mataifa, lakini ukawaeneza watu wetu katika nchi.
3 Kwa maana hawakupata umiliki wa nchi kwa upanga wao, wala mkono wao wenyewe haukuwaokoa; bali mkono wako wakuume, mkono wako, na nuru ya uso wako, na kwa sababu uliwaridhia.
4 Mungu, wewe ni Mfalme wangu, amuru ushindi kwa ajili ya Yakobo.
5 Kwa uweza wako tutawaangusha chini maadui zetu; kwa jina lako tutatembea juu yao, wale wanao inuka dhidi yetu.
6 Kwa maana sitauamini upinde wangu, wala upanga wangu hautaniokoa.
7 Bali wewe ndeye uliyetuokoa na adui zetu, na umewaaibisha wale watuchukiao.
8 Katika Mungu tumefanywa kujivuna siku zote, nasi tutalishukuru jina lako milele. Selah
9 Lakini sasa umetutupa na kutufedhehesha, na hauendi na majeshi yetu.
10 Umetufanya kuwakimbia maadui zetu; na wale watuchukiao huchukua vitu vyetu vya thamani kwa ajili yao wenyewe.
11 Umetufanya kama kondoo aliyeandaliwa kwa ajili ya chakula na umetutawanya kati ya mataifa.
12 Wewe unawauza watu wako bure; kwa kufanya hivyo haukupata faida.
13 Wewe umetufanya kukemewa na majirani zetu, kuchekwa, na kudhihakiwa na wale wanao tuzunguka.
14 Umetufaya kituko kati ya mataifa,.......................................................
15 Siku zote fedheha yangu iko mbele yangu, na aibu ya uso wangu imenifunika
16 kwa sababu ya sauti yake iliyo kemea na kutukana, kwa sababu ya adui na kisasi.
17 Yote haya yametupata sisi; bado hatukukusahau wewe wala kulikosea agano lako.
18 Mioyo yetu haikukengeuka; hatua zetu hazikuiacha njia yako.
19 Bali wewe umetuadhibu vikali katika mahali pa mbweha na kutufunika na uvuli wa mauti.
20 Ikiwa tumelisahau jina la Mungu wetu au kueneza mikono yetu kwa Mungu mgeni,
21 Mungu asingeligundua hili? Kwa maana yeye anazijua siri za moyo.
22 Hakika, kwa ajili ya jina lako tutauawa siku zote; tunahesabiwa kuwa kondoo kwa ajili ya kuchinjwa.
23 Bwana, amka, kwa nini unalala? Inuka, usitutupe moja kwa moja.
24 Kwa nini unaficha uso wako na kusahau mateso yetu na kukandamizwa kwetu?
25 Kwa maana tumeyeyushwa kwenye mavumbi; miili yetu imeshikamana na ardhi.
26 Inuka utusaidie na utuokoe kwa ajili ya uaminifu wa agano lako.