55
Kwa kiongozi wa muziki; kwenye vyombo vya nyuzi. Maschili ya Daudi.
1 Uyategee sikio maombi yangu, Mungu; nawe usijifiche mbali na kusihi kwangu.
2 Unitazame kwa makini na unijibu; Sina pumziko katika shida zangu
3 kwa sababu ya sauti ya adui zangu, kwa sababu ya ukandamizaji wa waovu; maana wananiletea matatizo na kunitesa wakiwa na hasira.
4 Moyo wangu wasumbuka ndani yangu, na hofu ya kifo imeniangukia.
5 Uwoga na kutetemeka kumenijia, nayo hofu imenielemea.
6 Nikasema, “Oh, kama tu ningekuwa na mabawa kama njiwa! Ningelipaa mbali na kupata pumziko.
7 Tazama, ningeenda mbali; ningekaa jangwani. Selah
8 Ningefanya haraka kuja mafichoni mwako kuzikimbia dhoruba na tufani.”
9 Uwaangamize, Bwana, vuruga lugha zao! Kwa maana nimeona vurugu na ugomvi katika mji.
10 Mchana na usiku wao huenda kwenye kuta zake; uchafu na ufisadi uko katikati yake.
11 Uovu uko katikati yake; ukandamizaji na uongo hauiachi mitaa yake.
12 Kwa maana hakuwa adui aliye nikemea, hivyo ningevumilia; wala ingekuwa ni yule aliye nichukia aliyejiinua mwenyewe dhidi yagu, hivyo ningejificha asinione.
13 Lakini ulikuwa wewe, mtu sawa na mimi, mwenzangu na rafiki yangu.
14 Tulikuwa na ushirika mtamu pamoja; tuliingia katika nyumba ya Mungu tukiwa na umati mkubwa.
15 Kifo na kiwapate ghafla; na washuke wakiwa hai kuzimuni, maana ndiko waishiko waovu, hapo hapo kati yao.
16 Lakini kwangu mimi, nitamwita Mungu, na Yahwe ataniokoa.
17 Wakati wa jioni, asubuhi na mchana ninalalamika na kuomboleza; yeye atasikia sauti yangu.
18 Kwa usalama kabisa atayaokoa maisha yangu na vita dhidi yangu, kwa maana wale waliopigana nami walikuwa ni wengi.
19 Mungu, yule unayetawala milele, atawasikia na kuwaaibisha wao. Selah Hawabadiliki, na hawamhofu Mungu.
20 Rafiki yangu ameinua mikono yake dhidi ya wale waliokuwa na amani naye; Hakuheshimu agano alilokuwa nalo.
21 Mdomo wake ulikuwa laini kama siagi, lakini moyo wake ulikuwa adui; maneno yake yalikuwa laini kuliko mafuta, lakini yalikuwa ni panga zilizochomolewa.
22 Umtwike mizigo yako Yahwe, naye atakusaidia; yeye hataruhusu mtu mwenye haki kuyumbayumba.
23 Bali wewe, Mungu, utawaleta waovu chini kwenye shimo la uharibifu; watu wenye kiu ya kumwaga damu na waongo hawataishi hata nusu ya maisha kama wengine, lakini mimi nitakuamini wewe.