6
Kwa kiongozi wa muziki; kwenye vyombo vya nyuzi, weka kwenye mtindo wa Sheminith. Zaburi ya Daudi.
1 Yahweh, usinikemee ukiwa na hasira au usiniadhibu katika gadhabu yako.
2 Unihurumie, Yahwe, kwa maana ni dhaifu; uniponye, Yahweh, kwa kuwa mifupa yangu ina tikisika.
3 Moyo wangu pia umesumbuka sana. Lakini wewe, Yahweh, mpaka lini hali hii itaendelea?
4 Rudi, Yahweh! uniokoe. Uniokoe kwa sababu ya uaminifu wa agano lako!
5 kwa kuwa kifoni hakuna kumbukumbu lako. Kuzimuni ni nani atakaye kushukuru?
6 Nimechoshwa na kuugua kwangu. Ninalowanisha kitanda changu kwa machozi usiku kucha; ninaosha kiti changu kwa machozi.
7 Macho yangu yanafifia kwa kulia sana; yanazidi kuwa dhaifu kwa sababu ya adaui zangu.
8 Ondokeni kwangu, nyote mtendao maovu; kwa kuwa Yahweh amesikia sauti ya kilio changu.
9 Yahweh amesikia malalamiko yangu kwa ajili ya huruma; Yahweh ameyapokea maombi yangu.
10 Maadui zangu wote wataaibishwa na kuteswa sana. Watarudi nyuma na ghafra kufedheheshwa.