63
Zaburi ya Daudi, wakati yeye alipokuwa katika jangwa la Yuda.
1 Mungu, wewe ni Mungu wangu! Ninakutafuta wewe kwa bidii, moyo wangu unakiu yako, mwili wangu unakutamani sana wewe, katika ukame na nchi iliyochoka mahali ambapo hakuna maji.
2 Hivyo nimekutafuta wewe katika watu watakatifu kuona nguvu zako na utukufu wako.
3 Kwa sababu uaminifu wa agano lako ni bora kuliko uhai, midomo yangu itakusifu wewe.
4 Hivyo nitakutukuza wewe niwapo hai; kwa jina lako nitainua mikono yangu juu.
5 Itakuwa kana kwamba nilikula mlo wa mafuta na wenye kunona, kwa midomo ya furaha kinywa changu kitakusifu wewe,
6 nikufikiripo kitandani mwangu na kukutafakari wewe wakati wa saa za usiku.
7 Kwa maana umekuwa msaada wangu, na katika uvuli wa mbawa zako ninafurahia.
8 Ninashikamana nawe; mkono wako wa kuume unanisaidia.
9 Lakini wale watafutao kuuharibu uhai wangu wataenda chini kwenye sehemu ya chini kabisa ya nchi;
10 watakabidhiwa kwa wale ambao mikono yao hutumia upanga, nao watakuwa chakula cha mbweha.
11 Bali mfalme atashangilia katika Mungu; yeyote anaye apa kupitia yeye atajivunia yeye, lakini vinywa ya wale wasemao uongo watanyamazishwa.