65
Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi. Wimbo wa Daudi.
1 Kwako wewe, Mungu katika Sayuni, sifa zetu za kungoja; viapo vyetu vitaletwa kwako.
2 Wewe usikiaye maombi yetu, miili yote itakuja kwako.
3 Maovu yanatutawala sisi; kama yalivyo makosa yetu, wewe utayasamehe.
4 Amebarikiwa mtu yule ambaye wewe huchagua kumsogeza karibu yako ili kwamba aishi hekaluni mwako. Tutatoshelezwa kwa uzuri wa nyumba yako, hekalu lako takatifu.
5 Katika haki wewe utatujibu sisi kwa kufanya mambo ya ajabu, Mungu wa wokovu wetu; wewe ambaye ni ujasiri wa mwisho wote wa nchi na wa wale walio mbali toka pande za bahari.
6 Kwa manaa ni wewe ndiye uliyeifanya milima imara, wewe ambaye umefungwa mkanda wa uweza.
7 Ni wewe unyamazishaye ngurumo za baharini; ngurumo za mawimbi yake, na vurugu za watu.
8 Wale wanaoishi sehemu za mwisho kabisa wa nchi wanaogopa ushahidi wa matendo yako; wewe hufanya mashariki na magharibi kushangilia.
9 Wewe huja kuisaidia nchi; unainyeshea inchi; wewe unaiimarisha nchi vizuri; mto wa Mungu umejaa maji; wewe humpa mwanadamu nafaka unapokuwa umekwisha iandaa nchi.
10 Wewe huyajaza matuta maji ya kutosha; wapasawazisha palipoinuka; wailainisha nchi kwa manyunyu ya mvua; waibariki mimea kati yao.
11 Umeuvika mwaka taji ya wema wako; mvumo wa mapito yako hudondosha unono katika nchi.
12 Majani ya nyikani hudondosha umande, na vilima vimevikwa furaha.
13 Malisho yamevishwa mifugo; mabonde pia yamefunikwa na nafaka; yanapiga kelele za shangwe, nayo yanaimba.