67
Kwa kiongozi wa muziki; kwenye vyombo vya nyuzi. zaburi, wimbo.
1 Mungu atuhurumie sisi na kutubariki na kufanya nuru ya uso wake ituangazie Selah
2 ili kwamba njia zako zijulikane nchi yote, wokovu wako kati ya mataifa yote.
3 Watu wakusifu wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe.
4 Oh, mataifa wafurahi na na kuimba kwa furaha, maana utawahukumu watu kwa haki na kuwaongoza mataifa walioko duniani.
5 Watu wakushukuru wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe.
6 Nchi imetoa mavuno yake na Mungu, Mungu wetu, ametubariki.
7 Mungu ametubariki sisi, na miisho yote ya dunia itamuheshimu yeye.