73
Zaburi ya Asafu.
1 Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, kwa wale walio na moyo safi.
2 Lakini kwangu mimi, kidogo tu miguu yangu iteleze; miguu yangu karibu iteleze kutoka kwangu
3 kwa sababu niliwaonea wivu wenye kiburi nilipoona mafanikio ya waovu.
4 Kwa maana hawana maumivu hadi kufa kwao, lakini wana nguvu na wameshiba.
5 Wako huru dhidi ya mizigo ya watu wengine; nao hawateswi kama watu wengine.
6 Kiburi kinawapamba kama mkufu kwenye shingo zao; jeuri huwavika kama vazi.
7 Katika upofu wa jinsi hii dhambi huja; mawazo maovu hupita mioyoni mwao.
8 Wao hudhihaki na kuongea kwa namna ya uovu; kwa kiburi chao hutishia mateso.
9 Wameweka vinywa vyao dhidi ya mbingu, na ndimi zao hutanga tanga duniani.
10 Kwa hiyo watu wake huwageukia na maji yaliyojaa hukaushwa.
11 Nao husema, “Mungu anajuaje? Yako maarifa kwake yeye aliye juu?”
12 Fahamu: watu hawa ni waovu; mara zote hawajali, wakifanyika matajiri na matajiri.
13 Hakika nimeutunza moyo wangu bure na nimenawa mikono yangu pasipo kukosa.
14 Maana mchana kutwa nimeteswa na kuadhibiwa kila asubuhi.
15 Kama ningesema, “Ningesema mambo haya,” kumbe nigewasaliti kizazi hiki cha watoto wenu.
16 Ingawa nilijaribu kuyaelewa mambo haya, yalikuwa ni magumu sana kwangu.
17 Ndipo nilipoingia patakatifu pa Mungu na kuelewa hatma yao.
18 Hakika wewe huwaweka penye utelezi; huwaangusha mpaka palipoharibika.
19 Jinsi gani wamekuwa ukiwa kwa muda mfupi! Wamefika mwisho nao wamemaliza kwa utisho.
20 Wao ni kama ndoto wakati wa mtu kuamka; Bwana, utakapo inuka, utazidharau ndoto zao.
21 Maana moyo wangu ulipata uchungu, nami nilijeruhiwa sana.
22 Nilikuwa mjinga na sijui neno; nilikuwa kama mnyama tu mbele yako.
23 Lakini mimi nipo pamoja nawe daima; umenishika mkono wa kuume.
24 Utaniongoza kwa shauri lako na baadaye utanipokea katika utukufu.
25 Ni nani niliye naye mbinguni isipokuwa wewe? Hakuna nimtamaniye duniani isipokuwa wewe.
26 Mwili wangu na moyo wangu huwa dhaifu, bali Mungu ndiye nguvu ya moyo wangu daima.
27 Wale walio mbali nawe wataangamia; utawaangamiza wote wasio waaminifu kwako.
28 Lakini mimi, linipasalo kufanya ni kumkaribia Mungu. Nimemfanya Bwana Yahwe kimbilio langu. Nami nitayatangaza matendo yako yote.