76
Kwa kiongozi wa muziki, kwenye vyombo vya nyuzi. zaburi ya Asafu, wimbo.
1 Mungu amefanya mwenyewe kujulikana katika Yuda; jina lake ni kuu katika Israeli.
2 Hema yake iko salemu; makao yake yako yako Sayuni.
3 Huko ndiko alivunja mishale ya upinde, ngao, upanga, na silaha zingine za vita. Selah
4 Wewe unang'aa sana na huufunua utukufu wako, ushukapo kutoka milimani, ambako uliwauwa mateka.
5 Wenye moyo shujaa walitekwa nyara; walilala mauti. Mashujaa wote walikuwa wanyonge.
6 Kwa kukemea kwako, ewe Mungu wa Yakobo, wote gari na farasi walilala mauti.
7 Wewe, ndiyo wewe, ni wa kuogopwa; ni nani awezaye kusimama mbele yako wakati ukiwa na hasira?
8 Kutoka mbinguni wewe uliifanya hukumu yako isikike; nchi iliogopa na ikaa kimya
9 wakati wewe, Mungu, ulipoinuka kutekeleza hukumu na kuwaokoa wote wa nchi walio onewa. Selah
10 Hakika hukumu ya hasira yako dhidi ya binadamu itakuletea wewe sifa; wewe hujifunga mwenyewe hasira yako iliyo baki.
11 Wekeni nadhiri kwa Yahwe Mungu wenu na kuzihifadhi. Nao wote wamzungukao yeye mleteeni zawadi yeye ambaye ni wa kuogopwa.
12 Yeye huzikata roho za wakuu; huogopwa na wafalme wa nchi.