27
1 Hii ni orodha ya familia za viongozi wa Israeli, wakuu wa maelfu na mamia, pamoja na maafisa wa jeshi walio mtumikia mfalme kwa namna tofauti. Kila kikosi cha jeshi kilitumika mwenzi hadi mwezi kwa mwaka mzima. Kila kikosi kilikuwa na wanaume elfu ishirini na nne.
2 Kwa mwezi wa kwanza wa kikosi alikuwa Yashobeamu mwana wa Zabdieli. Katika kikosi chake kulikuwa na wanaume elfu ishirini na nne.
3 Alikuwa miongoni mwa uzao wa Perezi na mhusika wa maafisa wa jeshi kwa mwezi wa kwanza.
4 Juu ya kikosi kwa mwezi wa pili alikuwa Dodai, wa ukoo wa uliotoka kwa Ahoa. Mikilothi alikuwa wa pili kwa cheo. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
5 Mkuu wa jeshi wa mwezi wa tatu alikuwa Benaia mwana wa Yehoiada, kuhani na kiongozi. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
6 Huyu ni Benaia aliye kuwa kiongozi wa wale thelathini na juu ya wale thelathini. Amizabadi mwanae alikuwa katika kikosi chake.
7 Mkuu kwa mwezi wa nne alikuwa Asaheli kaka wa Yoabu. Zebadia mwanae akawa mkuu baada yake. Katika kikosi chake kulikuwa na wanaume elfu ishirini na nne.
8 Mkuu kwa mwezi wa tano alikuwa Shamihuthi, mzao wa Izra. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
9 Mkuu kwa mwezi wa sita alikuwa Ira mwana wa Ikeshi, kutoka Tekoa. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
10 Mkuu kwa mwezi wa saba alikuwa Helezi Mpeloni, kutoka watu wa Efraimu. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
11 Mkuu kwa mwezi wa nane alikuwa Sibekai Mhushathi, kutoka ukoo ulitoka kwa Zera. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
12 Mkuu kwa mwezi wa tisa alikuwa Abi Ezeri Manathothi, kutoka kwa kabila la Benjamini. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
13 Mkuu kwa mwezi wa kumi alikuwa Maharai kutoka mji wa Netofa, kutoka ukoo ulio toka kwa Zera. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
14 Mkuu kwa mwezi wa kumi na moja alikuwa Benaia kutoka mji wa Pirathoni, kutoka kabila la Efraimu. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
15 Mkuu kwa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Helidai kutoka mji wa Netopafa, kutoka ukoo uliotoka kwa Othinieli. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
16 Hawa walikuwa viongozi wa makabila ya Israeli: Kwa kabila la Rubeni, Eliezeri mwana wa Zikri alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Simeoni, Shefatia mwana wa Maka alikuwa kiongozi.
17 Kwa kabila la Lawi, Hashinia mwana wa Kemueli alikuwa kiongozi, na Zadoki aliongoza uzao wa Aruni.
18 Kwa kabila la Yuda, Elihu, mmoja wa kaka zake Daudi, alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Isakari, Omri mwana wa Mikaeli alikuwa kiongozi.
19 Kwa kabila la Zebuluni, Ishimaia mwana wa Obadia alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Naftali, Yeremothi mwana wa Azirieli alikuwa kiongozi.
20 Kwa kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Azazia alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Manase, Yoeli mwana wa Pedaia alikuwa kiongozi.
21 Kwa nusu kabila la Manase lililo Gileadi, Ido mwana wa Zekaria alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Benjamini, Yaasieli mwana wa Abneri alikuwa kiongozi.
22 Kwa kabila la Dani, Azareli mwana wa Yerohamu alikuwa kiongozi. Hawa walikuwa viongozi wa makabila ya Israeli.
23 Daudi hakuwa hesabu wenye umri wa miaka ishirini au chini zaidi, kwasababu Yahweh alihaidi kuongeza Israeli kama nyota za mbinguni.
24 Yoabu mwana wa Zeruia alianza kuhesabu wanaume, lakini hakumaliza. Gadhabu iliangukia Israeli kwa hili. Hii idadi haikuandikwa kwenye nyakati za mfalme Daudi.
25 Azimavethi mwana wa Adieli alikuwa mhusika wa hazina za mfalme. Yonathani mwana wa Uzia alikuwa juu ya nyumba za ghala katika mashamba, kwenye miji, na vijijini, na kwenye minara iliyo imarishwa.
26 Ezri mwana wa Kelubi alikuwa juu ya mashamba, hao walio lima ardhi.
27 Shimei kutoka Rama alikuwa juu ya mashamba ya mizabibu, na Zabdi kutoka Shefamu alikuwa juu ya mizabibu na mhifadhi wa mvinyo.
28 Mwangalizi wa miti mizeituni na miti ya mikuyu iliyo kuwa bondeni alikuwa Baali Hanani kutoka Gederi, na juu ya nyumba za ghala za mafuta alikuwa Yoashi.
29 Juu ya mifugo iliyo kuwa inalishwa huko Sharoni alikuwa Shitrai kutoka Sharoni, na juu ya mifugo iliyo kuwa mabondeni alikuwa Shafati mwana wa Adlai.
30 Msimamizi wa ngamia alikuwa Obili Mishimaeli, na juu ya punda wakike alikuwa Yehideia kutoka Meronothi. Juu ya mifugo alikuwa Yazizi Mhagri.
31 Hawa wote walikuwa wasimamizi wa mali za Mfalme Daudi.
32 Yonathani, mjomba wake Daudi alikuwa mshauri, sababu alikuwa na busara na mwandishi. Yehieli mwana wa Hakimoni aliwajali watoto wa mfalme.
33 Ahithofeli alikuwa mshauri wa mfalme, na Hushai kutoka watu wa Waariki alikuwa mshauri wake wa siri.
34 Nafasi ya Ahithofeli ilichukuliwa na Yehoiada mwana wa Benaia, na Abiathari. Yoabu alikuwa mkuu wa jeshi la mfalme.