16
1 Namkabidhi kwenu Fibi dada yetu, ambaye ni mtumishi wa kanisa ambalo liko Kenkrea,
2 ili kwamba mnaweza kumpokea katika Bwana. Fanyeni hivi katika kicho cha thamani cha waumini, na msimame pamoja naye katika jambo lolote atakalokuwa na uhitaji nalo. Maana yeye mwenyewe amekuwa mhudumu wa wengi, na kwa ajili yangu mwenyewe.
3 Msalimu Priska na Akila, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu,
4 ambao kwa maisha yangu waliyahatarisha maisha yao wenyewe. Ninatoa shukrani kwao, na siyo tu mimi, bali pia kwa makanisa yote ya mataifa.
5 Lisalimie kanisa ambalo liko nyumbani kwao. Msalimie Epanieto mpendwa wangu, ambaye ni mzaliwa wa kwanza wa Kristo katika Asia.
6 Msalimie Mariamu ambaye ametenda kazi kwa bidii kwa ajili yenu.
7 Msalimie Androniko na Yunia, jamaa zangu, na wafungwa pamoja nami. Ni wa muhimu miongoni mwa mitume, ambao pia walitangulia kumjua Kristo kabla yangu.
8 Msalimie Ampliato, mpendwa wangu katika Bwana.
9 Msalimie Urbano, mtenda kazi pamoja nami katika Kristo, na Stakisi mpendwa wangu.
10 Msalimie Apele, mwenye kukubaliwa katika Kristo. Wasalimie wote ambao walio katika nyumba ya Aristobulo.
11 Nisalimie Herodioni, jamaa yangu. Nisalimie wote walio katika nyumba ya Narkiso, ambao wako katika Bwana.
12 Nisalimie Trifaina na Trifosa, wanaotenda kazi kwa bidii katika Bwana. msalimie Persisi mpendwa, ambaye ametenda kazi zaidi kwa Bwana,
13 Nisalimie Rufo, aliyechaguliwa katika Bwana na mama yake na wangu.
14 Msalimie Asinkrito, Flegon, Herme, Patroba, Herma, na ndugu wote walio pamoja nao.
15 Nisalimie Filologo naYulia, Nerea na dada yake, na Olimpa, na waumini wote walio pamoja nao.
16 Nisalimie kila mmoja kwa busu takatifu. Makanisa yote katika Kristo yawasalimu.
17 Sasa nawasihi, ndugu, kutafakari juu ya hao ambao wanasababisha mgawanyiko na vipingamizi. Wanakwenda kinyume na mafundisho ambayo mmekwisha kujifunza. Geukeni mtoke kwao.
18 Kwa maana watu kama hawa hawamtumikii Kristo Bwana, bali matumbo yao wenyewe. Kwa maneno yao laini na pongezi za uongo wanadanganya mioyo ya wasio na hatia.
19 Kwa mfano wa utii wenu mwamfikia kila mmoja. Kwa hiyo, nafurahi juu yenu, lakini nawataka ninyi mwe na busara katika hali ya wema, na kutokuwa na hatia mbele ya uovu.
20 Mungu wa amani hatakawia kumwangamiza shetani chini ya nyayo zenu. Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.
21 Timotheo, mtendakazi pamoja nami, awasalimu, na Lukio, Yasoni na Sospeter, jamaa zangu.
22 Mimi, Tertio, niliyeuandika waraka huu, nawasalimu katika jina la Bwana.
23 Gayo, aliyenitunza na kwa kanisa lote, lawasalimu. Erasto, mtunza hazina wa mji, awasalimu, pamoja na Kwarto aliye ndugu.
24 (Zingatia: Katika nakala halisi za kwanza, mstari huu haupo. Tazama Warumi 16: 20. “Neema ya Bwana Yesu Kristo ikae nanyi nyote. Amina.”)
25 Sasa kwake yeye aliye na uwezo kufanya msimame kulingana na injili na mafundisho ya Yesu Kristo, kulingana na ufunuo wa siri iliyofichwa kwa muda mrefu,
26 lakini sasa imekwisha funuliwa na kufanywa kujulikana na maandiko ya unabii kulingana na amri ya Mungu wa milele, kwa utii wa imani miongoni mwa mataifa yote?
27 Kwa Mungu pekee mwenye hekima, kupitia Yesu Kristo, kuwe na utukufu milele yote. Amina