Ruth
1
1 Ilitokea katika siku za utawala wa majaji kuwa kulikuwa na njaa katika nchi, na mtu mmoja wa Bethelehemu ya Yuda alikwenda katika nchi ya Moabu pamoja na mke wake na watoto wake walili wa kiume.
2 Jina la mtu huyo lilikuwa Elimeleki, na jina la mke wake lilikuwa Naomi. Majina ya watoto wake wawili wa kiume waliitwa Mahiloni na Kileoni, ambao walikuwa Waefraimu wa Betherehemu ya Yuda. Waliwasili katika nchi ya Moabu na kuishi hapo.
3 Ndipo Elimeleki, mume wa Naomi, alikufa, na Naomi aliachwa na watoto wake wa kiume wawili.
4 Watoto hawa walioa wanawake wa Moabu; jina la mmoja lilikuwa Oripa, na jina la mwingine lilikuwa Ruth. waliishi huko kwa takribani miaka kumi.
5 Kisha wote Mahiloni na Kileoni walikufa, na kumuacha Naomi bila mme wake na bila watoto wake wawili.
6 Ndipo Naomi aliamua kuondoka Moabu pamoja na wake wa watoto wake na kurudi Yuda kwa sababu alikuwa amesikia katika mkoa wa Moabu kuwa Yahweh amewasaidia watu wake katika uhitaji na amewapa chakula.
7 Hivyo aliondoka sehemu aliyokuwa pamoja na wake wa watoto wake wawili, walitelemka njia kurudi kwenye nchi ya Yuda.
8 Naomi aliwaambia wake wa watoto wake, “Nendeni, mrudi, kila mmoja wenu, kwenye nyumba ya mama yake. na Mungu aonyeshe wema juu yenu, kama mlivyo onyesha wema kwao waliokufa na kwangu.
9 Mungu awajalie ninyi kupata pumziko, kila mmoja wenu katika nyumba ya mme mwingine.” Kisha akawabusu, na wakapaza sauti zao na kulia.
10 Wakamwambia, “Hapana! tutarudi pamoja na wewe kwa watu wako.”
11 Lakini Naomi alisema, “Rudini, wanangu! Kwa nini mtakwenda na mimi? Kwani bado nina watoto katika tumbo langu kwa ajili yenu, ili kwamba waje wawe waume zenu?
12 Rudini, wanangu, nendeni katika njia zenu wenyewe, kwa kuwa mimi ni mzee sana kuwa na mme. Kama nikisema, 'Natumaini nipate mume usiku huu,' na kisha kuzaa watoto wakiume, kwa hiyo mnaweza kusubiri mpaka wakue?
13 Mtasubiri na msiolewe sasa? Hapana, wanangu! Ina nihuzunisha zaidi, kuliko inavyo wahuzunisha ninyi, kwa sababu mkono wa Yahweh umeenda kinyume na mimi.”
14 Ndipo wake wa watoto wake wakapaza sauti zao na kulia tena. Oripa alimuaga kwa kumbusu, lakini Ruth aliendelea kubaki naye.
15 Naomi alisema, “sikiliza, mwenzako amerudi kwa watu wake na miungu yake. Ruri pamoja naye.”
16 lakini Ruth alisema, “Usiniache niondoke mbali nawe, kwa kuwa uendako, nitakwenda, utakapoishi, nitaishi; watu wako watakuwa watu wangu, na Mungu wako atakuwa Mungu wangu.
17 Mahali utakapofia, nitafia hapo, na hapo nitazikwa. Yahweh aniwezeshe, na hata zaidi, ikiwa kuna chochote isipokuwa kifo kamwe hakiwezi kututenganisha.
18 Naomi alipoona kuwa Ruth alikuwa ameamua kwenda naye, aliacha kubishana naye.
19 Hivyo wote wawili walisafiri mpaka walipofika mjini Bethelehemu. Kwa hiyo walipofika Bethlehemu, mji wote uliwafurahia, wanawake walisema, “Huyu ni Naomi?”
20 Lakini aliwaambia, “Msiniite Naomi. Niiteni Mchungu, kwa kuwa Mwenyezi Mungu amenitenda mambo machungu sana.
21 Nilikwenda nikiwa nimejaa, lakini Yahweh kanirudisha nyumbani nikiwa sina wote. Hivyo kwa nini mnaniita Naomi, wakati mnaona Yahweh amenihukumu, kuwa Mwenyezi Mungu amenitaabisha?”
22 Kwa hivyo Naomi na Ruth Mmoabu, mke wa mtoto wake, walirudi kutoka nchi ya Moabu. walirudi Bethrehemu mwazo wa mavuno ya shairi.