24
Migawanyo Ya Makuhani
Hii ndiyo migawanyo ya wana wa Aroni:
Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari. Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, nao hawakuwa na wana; kwa hiyo ndugu zao Eleazari na Ithamari wakahudumu kama makuhani. Akisaidiwa na Sadoki mwana wa Eleazari na Ahimeleki mwana wa Ithamari, Daudi aliwapanga wazao wa Aroni katika migawanyo kufuatana na wajibu wa huduma zao. Idadi kubwa ya viongozi walipatikana miongoni mwa wazao wa Eleazari, kuliko miongoni mwa wazao wa Ithamari, nao waligawanywa kwa uwiano: Viongozi kumi na sita kutoka jamaa ya wazao wa Eleazari na viongozi wanane kutoka jamaa ya wazao wa Ithamari. Waliwagawanya bila upendeleo kwa kupiga kura, kwa kuwa kulikuwa na maafisa wa mahali patakatifu na maafisa wa Mungu miongoni mwa wazao wale wa Eleazari na wale wa Ithamari.
Mwandishi Shemaya mwana wa Nethaneli, Mlawi, aliorodhesha majina yao mbele ya Mfalme Daudi na maafisa: Kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi: jamaa moja ikitoka upande wa Eleazari na nyingine upande wa Ithamari.
 
Kura ya kwanza ilimwangukia Yehoyaribu,
ya pili Yedaya,
ya tatu Harimu,
ya nne Seorimu,
ya tano Malkiya,
ya sita Miyamini,
10 ya saba Hakosi,
ya nane Abiya,
11 ya tisa Yeshua,
ya kumi Shekania,
12 ya kumi na moja Eliashibu,
ya kumi na mbili Yakimu,
13 ya kumi na tatu Hupa,
ya kumi na nne Yeshebeabu,
14 ya kumi na tano Bilga,
ya kumi na sita Imeri,
15 ya kumi na saba Heziri,
ya kumi na nane Hapisesi,
16 ya kumi na tisa Pethahia,
ya ishirini Yehezkeli,
17 ya ishirini na moja Yakini,
ya ishirini na mbili Gamuli,
18 ya ishirini na tatu Delaya,
ya ishirini na nne Maazia.
 
19 Huu ulikuwa ndio utaratibu wao uliokubalika wa kuhudumu walipoingia katika Hekalu la Bwana kulingana na masharti waliyoelekezwa na Aroni baba yao, kama Bwana, Mungu wa Israeli, alivyokuwa amemwamuru.
Walawi Waliobaki
20 Kuhusu wazao wa Lawi waliobaki:
Kutoka kwa wana wa Amramu: alikuwa Shubaeli;
kutoka kwa wana wa Shubaeli: alikuwa Yedeya.
21 Kwa wa Rehabia, kutoka kwa wanawe:
Ishia alikuwa wa kwanza.
22 Kutoka kwa Waishari: alikuwa Shelomithi,
kutoka kwa wana wa Shelomithi: alikuwa Yahathi.
23 Wana wa Hebroni: Yeria alikuwa mkuu, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne.
24 Mwana wa Uzieli: alikuwa Mika;
kutoka kwa wana wa Mika: alikuwa Shamiri.
25 Ndugu yake Mika: alikuwa Ishia;
na kutoka kwa wana wa Ishia: alikuwa Zekaria.
26 Wana wa Merari: walikuwa Mahli na Mushi.
Mwana wa Yaazia: alikuwa Beno.
27 Wana wa Merari:
kutoka kwa Yaazia: ni Beno, Shohamu, Zakuri na Ibri.
28 Kutoka kwa Mahli: alikuwa Eleazari, ambaye hakuwa na wana.
29 Kutoka kwa Kishi: mwana wa Kishi:
alikuwa Yerameeli.
30 Nao wana wa Mushi: walikuwa Mahli, Ederi na Yeremothi.
 
Hawa walikuwa Walawi kulingana na jamaa zao. 31 Pia walipiga kura kama vile ndugu zao wazao wa Aroni walivyofanya, mbele ya Mfalme Daudi, Sadoki, Ahimeleki na mbele ya viongozi wa jamaa ya makuhani na ya Walawi. Jamaa za ndugu wakubwa zilitendewa sawasawa na zile za ndugu wadogo.