12
Orodha Ya Wafalme Walioshindwa
Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:
 
Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.
Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi. Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi*Yaani Bahari ya Galilaya. hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya ChumviYaani Bahari Mfu.), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga.
 
Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.
Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.
 
Mose, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.
 
Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao: nchi ya vilima, shefela, upande wa magharibi, Araba, materemko ya milima, jangwa, na Negebu; nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi):
 
mfalme wa Yeriko mmoja
mfalme wa Ai (karibu na Betheli) mmoja
10 mfalme wa Yerusalemu mmoja
mfalme wa Hebroni mmoja
11 mfalme wa Yarmuthi mmoja
mfalme wa Lakishi mmoja
12 mfalme wa Egloni mmoja
mfalme wa Gezeri mmoja
13 mfalme wa Debiri mmoja
mfalme wa Gederi mmoja
14 mfalme wa Horma mmoja
mfalme wa Aradi mmoja
15 mfalme wa Libna mmoja
mfalme wa Adulamu mmoja
16 mfalme wa Makeda mmoja
mfalme wa Betheli mmoja
17 mfalme wa Tapua mmoja
mfalme wa Heferi mmoja
18 mfalme wa Afeki mmoja
mfalme wa Lasharoni mmoja
19 mfalme wa Madoni mmoja
mfalme wa Hazori mmoja
20 mfalme wa Shimron-Meroni mmoja
mfalme wa Akishafu mmoja
21 mfalme wa Taanaki mmoja
mfalme wa Megido mmoja
22 mfalme wa Kedeshi mmoja
mfalme wa Yokneamu katika Karmeli mmoja
23 mfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori) Au: katika miinuko ya Nafoth-Dori. mmoja
mfalme wa Goimu katika Gilgali mmoja
24 mfalme wa Tirsa mmoja
wafalme jumla yao ilikuwa thelathini na mmoja.

*12:3 Yaani Bahari ya Galilaya.

12:3 Yaani Bahari Mfu.

12:23 Au: katika miinuko ya Nafoth-Dori.