2
Wana wa Israeli
Hawa walikuwa wana wa Israeli: Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Zabuloni, Dani, Yusufu, Benyamini, Naftali, Gadi na Asheri.
Yuda
Hadi wana wa Hesroni
Wana wa Yuda walikuwa:
Eri, Onani na Shela. Hawa watatu walizaliwa kwake na mkewe Mkanaani, binti Shua.
(Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni pa Mwenyezi Mungu, kwa hiyo Mwenyezi Mungu alimuua.)
Tamari, mkwewe Yuda, alimzalia wana wawili: Peresi na Zera.
Yuda alikuwa na jumla ya wana watano.
 
Wana wa Peresi walikuwa:
Hesroni na Hamuli.
Wana wa Zera walikuwa:
Zimri, Ethani, Hemani, Kalkoli na Darda. Jumla ya wana wa Zera walikuwa watano.
Mwana wa Karmi alikuwa:
Akari*maana yake Taabisha; pia anaitwa Akani (Yoshua 6:1-26; 22:20), ambaye alileta taabu kwa Waisraeli kwa kukiuka onyo la kutochukua vitu vilivyotengwa kwa ajili ya kuangamizwa.
Mwana wa Ethani alikuwa:
Azariya.
Wana wa Hesroni walikuwa:
Yerameeli, Ramu na Kalebu.
Kuanzia Ramu mwana wa Hesroni
10 Ramu alimzaa Aminadabu,
naye Aminadabu akamzaa Nashoni, kiongozi wa kabila la Yuda.
11 Nashoni akamzaa Salmoni,
Salmoni akamzaa Boazi,
12 Boazi akamzaa Obedi,
Obedi akamzaa Yese.
 
13 Yese akawazaa
Eliabu mwanawe wa kwanza; wa pili Abinadabu,
wa tatu Shimea, 14 wa nne Nethaneli,
wa tano Radai, 15 wa sita Osemu,
na wa saba Daudi.
16 Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili.
Wana wa Seruya walikuwa watatu: Abishai, Yoabu na Asaheli.
17 Abigaili alikuwa mama yake Amasa, ambaye baba yake alikuwa Yetheri Mwishmaeli.
Kalebu mwana wa Hesroni
18 Kalebu mwana wa Hesroni akazaa wana na mkewe Azuba (na pia na Yeriothi). Hawa ndio wana Azuba aliomzalia Kalebu:
Yesheri, Shobabu na Ardoni.
19 Azuba alipofariki, Kalebu akamwoa Efrata, aliyemzalia Huri.
20 Huri akamzaa Uri, naye Uri akamzaa Bezaleli.
 
21 Hatimaye, Hesroni alipokuwa na umri wa miaka sitini, alimwoa binti Makiri, babaye Gileadi. Akakutana kimwili naye, akamzalia Segubu.
22 Segubu akamzaa Yairi, ambaye alitawala miji ishirini na tatu katika Gileadi.
23 (Lakini Geshuri na Aramu wakateka miji ya Hawoth-Yairi, pamoja na Kenathi na makazi yake; jumla ilikuwa miji sitini.)
Wote hawa walikuwa wazao wa Makiri babaye Gileadi.
24 Baada ya Hesroni kufa huko Kalebu-Efrata, Abiya mjane wa Hesroni akamzalia Ashuru, aliye baba wa Tekoa.
Yerameeli mwana wa Hesroni
25 Wana wa Yerameeli mzaliwa wa kwanza wa Hesroni walikuwa:
Ramu mzaliwa wake wa kwanza, Buna, Oreni, Osemu na Ahiya. 26 Yerameeli alikuwa na mke mwingine, aliyeitwa Atara, aliyekuwa mama yake Onamu.
27 Wana wa Ramu mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli walikuwa:
Maasi, Yamini na Ekeri.
28 Wana wa Onamu walikuwa:
Shamai na Yada.
Wana wa Shamai walikuwa:
Nadabu na Abishuri. 29 Mke wa Abishuri aliitwa Abihaili, aliyemzalia Abani na Molidi.
30 Wana wa Nadabu walikuwa
Seledi na Apaimu, lakini Seledi alikufa bila kuzaa watoto.
31 Apaimu akamzaa:
Ishi aliyekuwa baba wa Sheshani.
Sheshani akamzaa Alai.
32 Wana wa Yada, nduguye Shamai walikuwa:
Yetheri na Yonathani. Yetheri alikufa bila kuzaa watoto.
33 Wana wa Yonathani walikuwa:
Pelethi na Zaza.
Hao walikuwa wazao wa Yerameeli.
 
34 Sheshani hakuwa na watoto wa kiume, ila watoto wa kike tu.
Alikuwa na mtumishi Mmisri aliyeitwa Yarha. 35 Sheshani akamwoza huyu mtumishi wake Yarha binti yake, akamzalia mwana jina lake Atai.
36 Atai akamzaa Nathani,
Nathani akamzaa Zabadi,
37 Zabadi akamzaa Eflali,
Eflali akamzaa Obedi,
38 Obedi akamzaa Yehu,
Yehu akamzaa Azaria,
39 Azaria akamzaa Helesi,
Helesi akamzaa Eleasa,
40 Eleasa akamzaa Sismai,
Sismai akamzaa Shalumu,
41 Shalumu akamzaa Yekamia,
naye Yekamia akamzaa Elishama.
Koo za Kalebu
42 Wana wa Kalebu nduguye Yerameeli walikuwa:
Mesha mzaliwa wake wa kwanza alimzaa Zifu,
naye mwanawe Maresha akamzaa Hebroni.
43 Hebroni alikuwa na wana wanne:
Kora, Tapua, Rekemu na Shema.
44 Shema alikuwa baba yake Rahamu na Rahamu alikuwa baba wa Yorkeamu
na Rekemu alikuwa baba wa Shamai.
45 Shamai akamzaa Maoni,
naye Maoni akamzaa Beth-Suri.
46 Efa, suria wa Kalebu aliwazaa:
Harani, Mosa na Gazezi.
Harani alikuwa baba wa Gazezi.
47 Wana wa Yadai walikuwa:
Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa na Shaafu.
48 Maaka suria wa Kalebu alikuwa mamaye
Sheberi na Tirhana.
49 Pia Maaka akamzaa Shaafu babaye Madmana,
na Sheva babaye Makbena na Gibea.
Kalebu alikuwa na binti jina lake Aksa.
50 Hao walikuwa wazao wa Kalebu.
 
Wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata, walikuwa:
Shobali akamzaa Kiriath-Yearimu, 51 Salma akamzaa Bethlehemu, naye Harefu akamzaa Beth-Gaderi.
52 Wazao wa Shobali, baba yake Kiriath-Yearimu, walikuwa:
Haroe, nusu ya Wamenuhothi, 53 pamoja na koo za Kiriath-Yearimu ambazo ni: Waithiri, Waputhi, Washumathi na Wamishrai. Kutokana na watu hawa walizaliwa Wasorathi na Waeshtaoli.
54 Wazao wa Salma walikuwa:
Bethlehemu, Wanetofathi, Atroth-Beth-Yoabu, nusu ya Wamanahathi, Wazori, 55 pamoja na koo za waandishi zilizoishi katika mji wa Yabesi: yaani Watirathi, Washimeathi na Wasukathi. Hawa ndio Wakeni waliotokana na Hamathi, baba wa nyumba ya Rekabu.

*2:7 maana yake Taabisha; pia anaitwa Akani (Yoshua 6:1-26; 22:20)