6
Wana wa Lawi
Wana wa Lawi walikuwa:
Gershoni, Kohathi na Merari.
Wana wa Kohathi walikuwa:
Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
Amramu alikuwa na wana:
Haruni, Musa, na Miriamu.
Haruni alikuwa na wana:
Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.
Eleazari akamzaa Finehasi,
Finehasi akamzaa Abishua,
Abishua akamzaa Buki,
Buki akamzaa Uzi,
Uzi akamzaa Zerahia,
Zerahia akamzaa Merayothi,
Merayothi akamzaa Amaria,
Amaria akamzaa Ahitubu,
Ahitubu akamzaa Sadoki,
Sadoki akamzaa Ahimaasi,
Ahimaasi akamzaa Azaria,
Azaria akamzaa Yohanani,
10 Yohanani akamzaa Azaria (ndiye alifanya kazi ya ukuhani katika Hekalu alilojenga Mfalme Sulemani huko Yerusalemu),
11 Azaria akamzaa Amaria,
Amaria akamzaa Ahitubu,
12 Ahitubu akamzaa Sadoki,
Sadoki akamzaa Shalumu,
13 Shalumu akamzaa Hilkia,
Hilkia akamzaa Azaria,
14 Azaria akamzaa Seraya,
Seraya akamzaa Yehosadaki.
15 Yehosadaki alihamishwa wakati Mwenyezi Mungu aliwapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa mkono wa Mfalme Nebukadneza.
 
16 Wana wa Lawi walikuwa:
Gershoni, Kohathi na Merari.
17 Haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni:
Libni na Shimei.
18 Wana wa Kohathi walikuwa:
Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
19 Wana wa Merari walikuwa:
Mahli na Mushi.
 
Zifuatazo ni koo za Walawi wakiorodheshwa kufuatana na baba zao:
20 Wazao wa Gershoni:
Gershoni akamzaa Libni, Libni akamzaa Yahathi,
Yahathi akamzaa Zima, 21 Zima akamzaa Yoa,
Yoa akamzaa Ido, Ido akamzaa Zera,
Zera akamzaa Yeatherai.
22 Wazao wa Kohathi:
Kohathi akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Kora,
Kora akamzaa Asiri, 23 Asiri akamzaa Elkana,
Elkana akamzaa Ebiasafu, Ebiasafu akamzaa Asiri,
24 Asiri akamzaa Tahathi, Tahathi akamzaa Urieli,
Urieli akamzaa Uzia, Uzia akamzaa Shauli.
25 Wazao wa Elkana walikuwa:
Amasai na Ahimothi,
26 Ahimothi akamzaa Elkana, Elkana akamzaa Sofai,
Sofai akamzaa Nahathi, 27 Nahathi akamzaa Eliabu,
Eliabu akamzaa Yerohamu, Yerohamu akamzaa Elkana,
Elkana akamzaa Samweli.
28 Wana wa Samweli walikuwa:
Yoeli mzaliwa wake wa kwanza,
na Abiya mwanawe wa pili.
29 Wafuatao ndio wazao wa Merari:
Merari akamzaa Mahli, Mahli akamzaa Libni,
Libni akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Uza,
30 Uza akamzaa Shimea, Shimea akamzaa Hagia,
Hagia akamzaa Asaya.
Waimbaji wa Hekalu
31 Hawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko. 32 Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, hadi hapo Mfalme Sulemani alipojenga Hekalu la Mwenyezi Mungu huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.
 
33 Wafuatao ni watu waliohudumu pamoja na wana wao:
 
Kutoka koo za Wakohathi walikuwa:
Hemani, mpiga kinanda,
alikuwa mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli,
34 mwana wa Elkana, mwana wa Yerohamu,
mwana wa Elieli, mwana wa Toa,
35 mwana wa Sufu, mwana wa Elkana,
mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai,
36 mwana wa Elkana, mwana wa Yoeli,
mwana wa Azaria, mwana wa Sefania,
37 mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri,
mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora,
38 mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi,
mwana wa Lawi, mwana wa Israeli;
39 na msaidizi wa Hemani alikuwa Asafu, aliyesimama mkono wa kuume:
Asafu mwana wa Berekia, mwana wa Shimea,
40 mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya,
mwana wa Malkiya, 41 mwana wa Ethni,
mwana wa Zera, mwana wa Adaya,
42 mwana wa Ethani, mwana wa Zima,
mwana wa Shimei, 43 mwana wa Yahathi,
mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi.
44 Na kutoka kwa walioshirikiana nao, Wamerari, mkono wake wa kushoto:
Ethani mwana wa Kishi, mwana wa Abdi,
mwana wa Maluki, 45 mwana wa Hashabia,
mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia,
46 mwana wa Amzi, mwana wa Bani,
mwana wa Shemeri, 47 mwana wa Mahli,
mwana wa Mushi, mwana wa Merari,
mwana wa Lawi.
 
48 Ndugu zao wengine Walawi walipewa huduma nyingine za kuhudumia hema takatifu, nyumba ya Mungu.
49 Lakini Haruni na uzao wake ndio walikuwa na wajibu wa kutoa sadaka katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba pamoja na yote yaliyofanyika pa Patakatifu, wakifanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, sawasawa na yale yote aliyoagiza Musa mtumishi wa Mungu.
 
50 Hawa walikuwa wazao wa Haruni:
Haruni akamzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Finehasi,
Finehasi akamzaa Abishua, 51 Abishua akamzaa Buki,
Buki akamzaa Uzi, Uzi akamzaa Zerahia,
52 Zerahia akamzaa Merayothi, Merayothi akamzaa Amaria,
Amaria akamzaa Ahitubu, 53 Ahitubu akamzaa Sadoki,
Sadoki akamzaa Ahimaasi.
 
54 Zifuatazo ni sehemu walizopewa ziwe nchi yao kwa ajili ya makazi yao (walipewa wazao wa Haruni waliotoka katika ukoo wa Wakohathi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia):
55 Walipewa Hebroni katika nchi ya Yuda pamoja na maeneo ya malisho yanayouzunguka. 56 Lakini mashamba pamoja na vijiji vilivyouzunguka mji alipewa Kalebu mwana wa Yefune. 57 Kwa hiyo wazao wa Haruni walipewa miji ifuatayo: Hebroni (mji wa makimbilio), Libna, Yatiri, Eshtemoa, 58 Hileni, Debiri, 59 Ashani, Yuta na Beth-Shemeshi pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
60 Kutoka kabila la Benyamini, walipewa Gibeoni, Geba, Alemethi na Anathothi, pamoja na maeneo yake ya malisho.
Miji hii kumi na tatu iligawanywa miongoni mwa koo za Wakohathi.
 
61 Wazao waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za nusu ya kabila la Manase.
62 Wazao wa Gershoni, kufuatana na koo zao, walipewa miji kumi na tatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri na Naftali, na kutoka sehemu ya kabila la Manase huko Bashani.
63 Wazao wa Merari, kufuatana na koo zao walipewa miji kumi na mbili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni.
 
64 Kwa hiyo Waisraeli waliwapa Walawi miji hii pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
 
65 Kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini walipewa miji iliyotajwa hapo juu.
 
66 Baadhi ya koo za Wakohathi walipewa kama nchi yao miji kutoka kabila la Efraimu.
67 Katika nchi ya vilima ya Efraimu, walipewa Shekemu (mji wa makimbilio) na Gezeri, 68 Yokmeamu, Beth-Horoni, 69 Aiyaloni na Gath-Rimoni, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
70 Kutoka nusu ya kabila la Manase, Waisraeli waliwapa koo za Wakohathi waliobaki miji ya Aneri na Bileamu pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
 
71 Wagershoni walipokea miji ifuatayo:
Katika nusu ya kabila la Manase, walipokea Golani katika Bashani, na pia Ashtarothi, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
72 Kutoka kabila la Isakari walipokea Kedeshi, Daberathi, 73 Ramothi na Anemu, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
74 Kutoka kabila la Asheri, walipokea Mashali, Abdoni, 75 Hukoki na Rehobu, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
76 Kutoka kabila la Naftali, walipokea Kedeshi katika Galilaya, Hamoni na Kiriathaimu, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
 
77 Wamerari (Walawi waliobakia) walipokea miji ifuatayo:
kutoka kabila la Zabuloni, walipokea Yokneamu, Karta, Rimoni na Tabori, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
78 Kutoka kabila la Reubeni, ng’ambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko, walipokea Bezeri ulioko jangwani, Yahasa, 79 Kedemothi na Mefaathi, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
80 Na kutoka kabila la Gadi, walipokea Ramothi huko Gileadi, Mahanaimu, 81 Heshboni na Yazeri, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.