8
Ukoo wa Sauli Mbenyamini
Benyamini akamzaa:
Bela mzaliwa wake wa kwanza,
Ashbeli mwanawe wa pili, Ahara mwanawe wa tatu,
Noha mwanawe wa nne na Rafa mwanawe wa tano.
Wana wa Bela walikuwa:
Adari, Gera, Abihudi, Abishua, Naamani, Ahoa, Gera, Shefufani na Huramu.
Hawa ndio wazao wa Ehudi, waliokuwa viongozi wa jamaa za wale walioishi huko Geba na ambao walihamishiwa Manahathi:
Naamani, Ahiya na Gera. Gera ndiye aliwapeleka uhamishoni, na alikuwa baba yao Uza na Ahihudi.
Shaharaimu aliwazaa wana katika nchi ya Moabu baada ya kuwapa talaka wake zake wawili yaani Hushimu na Baara. Kwa mkewe Hodeshi, akawazaa wana saba: Yobabu, Sibia, Mesha, Malkamu, 10 Yeuzi, Sakia na Mirma. Hao walikuwa wanawe, viongozi wa jamaa zao. 11 Hushimu alimzalia: Abitubu na Elpaali.
12 Wana wa Elpaali walikuwa:
Eberi, Mishamu, Shemedi (aliyeijenga miji ya Ono na Lodi, pamoja na vijiji vyake), 13 na Beria na Shema, waliokuwa viongozi wa zile jamaa zilizokuwa zinaishi katika mji wa Aiyaloni, na ambao waliwafukuza wenyeji wa Gathi.
14 Wana wa Beria walikuwa Ahio, Shashaki, Yeremothi, 15 Zebadia, Aradi, Ederi, 16 Mikaeli, Ishpa, na Yoha.
17 Zebadia, Meshulamu, Hizki, Heberi, 18 Ishmerai, Izlia na Yobabu ndio walikuwa wana wa Elpaali.
19 Yakimu, Zikri, Zabdi, 20 Elienai, Silethai, Elieli, 21 Adaya, Beraya na Shimrathi walikuwa wana wa Shimei.
22 Wana wa Shashaki walikuwa Ishpani, Eberi, Elieli, 23 Abdoni, Zikri, Hanani, 24 Hanania, Elamu, Anthothiya, 25 Ifdeya na Penueli.
26 Shamsherai, Sheharia, Athalia, 27 Yaareshia, Ilya na Zikri walikuwa wana wa Yerohamu.
28 Hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa zao wakuu, kama walivyoorodheshwa katika koo zao, nao waliishi Yerusalemu.
 
29 Yeieli alikuwa baba yake Gibeoni naye aliishi huko Gibeoni.
Mke wake aliitwa Maaka. 30 Mwanawe mzaliwa wa kwanza alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Suri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu, 31 Gedori, Ahio, Zekeri, 32 na Miklothi aliyekuwa baba yake Shimea. Hawa pia waliishi karibu na jamaa zao huko Yerusalemu.
33 Neri akamzaa Kishi, Kishi akamzaa Sauli, Sauli akamzaa Yonathani, Malki-Shua, Abinadabu na Esh-Baali.
34 Yonathani akamzaa:
Merib-Baali*au Mefiboshethi, maana yake Mtu wa Aibu (taz. 2 Samweli 4:4)., naye Merib-Baali akamzaa Mika.
35 Wana wa Mika walikuwa:
Pithoni, Meleki, Tarea na Ahazi.
36 Ahazi akamzaa Yehoada. Naye Yehoada akawazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri, naye Zimri akamzaa Mosa. 37 Mosa akamzaa Binea; Refaya alikuwa mwanawe Binea, Eleasa mwanawe Refaya, naye Aseli mwanawe Eleasa.
38 Aseli alikuwa na wana sita; haya ndiyo majina yao:
Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Hawa wote ndio walikuwa wana wa Aseli.
39 Wana wa Esheki, nduguye Aseli, walikuwa:
Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Ulamu, wa pili Yeushi na wa tatu Elifeleti. 40 Wana wa Ulamu walikuwa mashujaa hodari walioweza kutumia upinde. Alikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla yao mia moja na hamsini.
Hawa wote ndio walikuwa wazao wa Benyamini.
 

*8:34 au Mefiboshethi, maana yake Mtu wa Aibu (taz. 2 Samweli 4:4).