27
Yothamu mfalme wa Yuda
(2 Wafalme 15:32-38)
Yothamu alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. Mama yake aliitwa Yerusha binti Sadoki. Akafanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu kama Uzia baba yake alivyokuwa amefanya, lakini tofauti na yeye, hakuingilia huduma za hekaluni mwa Mwenyezi Mungu. Lakini hata hivyo, watu wakaendelea na desturi zao mbaya. Yothamu akajenga upya Lango la Juu la Hekalu la Mwenyezi Mungu na kufanya kazi kubwa kwenye ukuta katika kilima cha Ofeli. Akajenga miji katika nchi ya vilima ya Yuda, pamoja na ngome na minara mwituni.
Yothamu akafanya vita na mfalme wa Waamoni na kumshinda. Mwaka ule Waamoni wakamlipa talanta mia moja*Talanta 100 za fedha ni sawa na tani 3.75. za fedha, kori elfu kumiKori 10,000 za ngano ni sawa na tani 2.2. za ngano, na kori elfu kumi za shayiri. Waamoni wakamletea kiasi hicho hicho mwaka wa pili na wa tatu.
Yothamu akaendelea kuwa na nguvu kwa sababu alienenda kwa ukamilifu mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wake.
Matukio mengine ya utawala wa Yothamu, pamoja na vita vyake vyote na vitu vingine alivyofanya, vimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda. Alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. Yothamu akalala na baba zake na akazikwa katika Mji wa Daudi. Naye Ahazi mwanawe akawa mfalme baada yake.

*27:5 Talanta 100 za fedha ni sawa na tani 3.75.

27:5 Kori 10,000 za ngano ni sawa na tani 2.2.