2
Orodha ya watu waliorudi kutoka uhamishoni
(Nehemia 7:4-73)
Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana):
 
Orodha ya wanaume kati ya watu wa Israeli ilikuwa:
wazao wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili (2,172);
wazao wa Shefatia, mia tatu sabini na wawili (372);
wazao wa Ara, mia saba sabini na watano (775);
wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu), elfu mbili mia nane na kumi na wawili (2,812);
wazao wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne (1,254);
wazao wa Zatu, mia tisa arobaini na watano (945);
wazao wa Zakai, mia saba na sitini (760);
10 wazao wa Bani, mia sita arobaini na wawili (642);
11 wazao wa Bebai, mia sita ishirini na watatu (623);
12 wazao wa Azgadi, elfu moja mia mbili ishirini na wawili (1,222);
13 wazao wa Adonikamu, mia sita sitini na sita (666);
14 wazao wa Bigwai, elfu mbili hamsini na sita (2,056);
15 wazao wa Adini, mia nne hamsini na wanne (454);
16 wazao wa Ateri (kupitia Hezekia), tisini na nane (98);
17 wazao wa Besai, mia tatu ishirini na watatu (323);
18 wazao wa Yora, mia moja na kumi na wawili (112);
19 wazao wa Hashumu, mia mbili na ishirini na watatu (223);
20 wazao wa Gibari, tisini na watano (95);
21 watu wa Bethlehemu, mia moja ishirini na watatu (123);
22 watu wa Netofa, hamsini na sita (56);
23 watu wa Anathothi, watu mia moja ishirini na nane (128);
24 watu wa Azmawethi, arobaini na wawili (42);
25 wazao wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi, mia saba arobaini na watatu (743);
26 wazao wa Rama na Geba, mia sita ishirini na mmoja (621);
27 watu wa Mikmashi, mia moja ishirini na wawili (122);
28 watu wa Betheli na Ai, mia mbili na ishirini na watatu (223);
29 wazao wa Nebo, hamsini na wawili (52);
30 wazao wa Magbishi, mia moja hamsini na sita (156);
31 wazao wa Elamu ile ingine, elfu moja mia mbili hamsini na wanne (1,254);
32 wazao wa Harimu, mia tatu na ishirini (320);
33 wazao wa Lodi, Hadidi na Ono, mia saba ishirini na watano (725);
34 wazao wa Yeriko, mia tatu arobaini na watano (345);
35 wazao wa Senaa, elfu tatu mia sita na thelathini (3,630).
 
36 Makuhani:
wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua), mia tisa sabini na watatu (973);
37 wazao wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili (1,052);
38 wazao wa Pashuri, elfu moja mia mbili arobaini na saba (1,247);
39 wazao wa Harimu, elfu moja na kumi na saba (1,017).
 
40 Walawi:
wazao wa Yeshua na Kadmieli (kupitia jamaa ya Hodavia), sabini na wanne (74).
 
41 Waimbaji:
wazao wa Asafu, mia moja ishirini na nane (128).
 
42 Mabawabu wa lango la Hekalu:
wazao wa Shalumu, Ateri, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai, mia moja thelathini na tisa (139).
 
43 Watumishi wa Hekalu*yaani Wanethini (pia 2:58, 70).:
wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,
44 wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni,
45 wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu,
46 wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani,
47 wazao wa Gideli, Gahari, Reaya,
48 wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu,
49 wazao wa Uza, Pasea, Besai,
50 wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu,
51 wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,
52 wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,
53 wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,
54 wazao wa Nesia na Hatifa.
 
55 Wazao wa watumishi wa Sulemani:
wazao wa Sotai, Hasaferethi, Peruda,
56 wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,
57 wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami.
58 Watumishi wa Hekalu, na wazao wa watumishi wa Sulemani, mia tatu tisini na wawili (392).
 
59 Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:
60 wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda, mia sita hamsini na wawili (652).
 
61 Kutoka miongoni mwa makuhani:
Wazao wa Hobaya, Hakosi, Barzilai (mtu aliyemwoa binti Barzilai Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).
62 Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa ukuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. 63 Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na ThumimuUrimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha kifuani cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha..
 
64 Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa elfu arobaini na mbili na mia tatu na sitini (42,360); 65 tena zaidi ya hao walikuwa na watumwa wa kiume na wa kike elfu saba, mia tatu na thelathini na saba (7,337); pia walikuwa na waimbaji wanaume na wanawake mia mbili. 66 Walikuwa na farasi mia saba thelathini na sita (736), nyumbu mia mbili arobaini na watano (245), 67 ngamia mia nne thelathini na watano (435), na punda elfu sita, mia saba na ishirini (6,720).
 
68 Walipofika kwenye nyumba ya Mwenyezi Mungu huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake. 69 Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni elfu sitini na mojaDarkoni 61,000 za dhahabu ni sawa na kilo 500. za dhahabu, mane elfu tano§Mane 5,000 za fedha ni sawa na kilo 2,900. za fedha, na mavazi mia moja ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo.
70 Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao.

*2:43 yaani Wanethini (pia 2:58, 70).

2:63 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha kifuani cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.

2:69 Darkoni 61,000 za dhahabu ni sawa na kilo 500.

§2:69 Mane 5,000 za fedha ni sawa na kilo 2,900.