35
Yakobo arudi Betheli
Kisha Mungu akamwambia Yakobo, “Panda uende Betheli ukakae huko. Ukamjengee Mungu madhabahu huko, Yeye aliyekutokea ulipokuwa unamkimbia Esau ndugu yako.”
Hivyo Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake pamoja na wote waliokuwa naye, “Iondoeni miungu ya kigeni mliyo nayo, mjitakase na mkabadilishe nguo zenu. Kisha njooni, twende Betheli, mahali nitakapomjengea Mungu madhabahu, aliyenijibu katika siku ya shida yangu, ambaye amekuwa pamoja nami popote nilipoenda.” Kwa hiyo wakampa Yakobo miungu yote ya kigeni waliyokuwa nayo, pamoja na pete zilizokuwa masikioni mwao. Yakobo akavizika chini ya mwaloni ulio Shekemu. Kisha wakaondoka, na utisho wa Mungu ukaipata miji yote iliyowazunguka. Kwa hiyo hakuna aliyewafuatia wana wa Yakobo.
Yakobo na watu wote waliokuwa pamoja naye wakafika Luzu (ndio Betheli), katika nchi ya Kanaani. Huko akajenga madhabahu na akapaita mahali pale El-Betheli*maana yake Mungu wa Betheli, kwa sababu mahali pale ndipo Mungu alijifunua kwake alipokuwa akimkimbia ndugu yake.
Wakati huu Debora, mlezi wa Rebeka, akafa na akazikwa chini ya mwaloni ulio nje ya Betheli. Kwa hiyo pakaitwa Alon-Bakuthimaana yake Mwaloni wa kilio.
Baada ya Yakobo kurudi kutoka Padan-Aramu, Mungu alimtokea tena na kumbariki. 10 Mungu akamwambia, “Jina lako ni Yakobomaana yake Ashikaye kisigino, au Atwaaye mahali pa mwingine, au Mdanganyaji. Lakini hutaitwa tena Yakobo; jina lako litakuwa Israeli§maana yake Yeye ashindanaye na Mungu.” Kwa hiyo akamwita Israeli.
11 Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi*Kiebrania El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote).; ukazae na kuongezeka. Taifa na jamii ya mataifa itatoka kwako, nao wafalme watatoka viunoni mwako. 12 Nchi niliyowapa Ibrahimu na Isaka nakupa wewe pia, nami nitawapa wazao wako baada yako.” 13 Kisha Mungu akapanda juu kutoka kwake mahali pale alipozungumza naye.
14 Yakobo akasimamisha nguzo ya jiwe mahali pale Mungu alipozungumza naye, akamimina sadaka ya kinywaji juu yake, pia akamimina mafuta juu yake. 15 Yakobo akapaita mahali pale Mungu alipozungumza naye Bethelimaana yake Nyumba ya Mungu.
Vifo vya Raheli na Isaka
16 Kisha wakaondoka Betheli. Kabla hawajafika Efrata, Raheli akaanza kujifungua na akapata shida kuu. 17 Alipokuwa katika shida hii katika kujifungua, mkunga akamwambia, “Usiogope, kwa sababu umempata mwana mwingine.” 18 Hapo alipopumua pumzi yake ya mwisho, kwa maana alikuwa akifa, akamwita mwanawe jina Benonimaana yake Mwana wa huzuni yangu. Lakini babaye akamwita jina Benyamini§maana yake Mwana wa mkono wangu wa kuume.
19 Kwa hiyo Raheli akafa, na akazikwa kando ya njia iendayo Efrata (ndio Bethlehemu). 20 Yakobo akasimamisha nguzo juu ya kaburi lake, ambayo hadi leo inatambulisha kaburi la Raheli.
21 Israeli akaendelea tena na safari yake na kupiga hema baada ya kupita Mnara wa Ederi. 22 Israeli alipokuwa akiishi katika nchi ile, Reubeni mwanawe alikutana kimwili na suria wa baba yake aliyeitwa Bilha, naye Israeli akasikia jambo hilo.
 
Yakobo alikuwa na wana kumi na wawili:
 
23 Wana wa Lea walikuwa:
Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo,
Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari na Zabuloni.
24 Wana wa Raheli walikuwa:
Yusufu na Benyamini.
25 Wana waliozaliwa na Bilha mjakazi wa Raheli walikuwa:
Dani na Naftali.
26 Wana waliozaliwa na Zilpa mjakazi wa Lea walikuwa:
Gadi na Asheri.
 
Hawa walikuwa wana wa Yakobo, waliozaliwa kwake akiwa Padan-Aramu.
 
27 Yakobo akarudi nyumbani mwa baba yake Isaka huko Mamre, karibu na Kiriath-Arba (yaani Hebroni), ambapo walikuwa wameishi Ibrahimu na Isaka. 28 Isaka aliishi miaka mia moja na themanini. 29 Kisha Isaka akapumua pumzi yake ya mwisho, akafa; akakusanywa pamoja na watu wake akiwa mzee aliyeshiba siku. Nao Esau na Yakobo, wanawe, wakamzika.

*35:7 maana yake Mungu wa Betheli

35:8 maana yake Mwaloni wa kilio

35:10 maana yake Ashikaye kisigino, au Atwaaye mahali pa mwingine, au Mdanganyaji

§35:10 maana yake Yeye ashindanaye na Mungu

*35:11 Kiebrania El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote).

35:15 maana yake Nyumba ya Mungu

35:18 maana yake Mwana wa huzuni yangu

§35:18 maana yake Mwana wa mkono wangu wa kuume