Hosea
1
Neno la Mwenyezi Mungu lililomjia Hosea mwana wa Beeri wakati wa utawala wa Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda, na wakati wa utawala wa Yeroboamu mwana wa Yehoashi, mfalme wa Israeli.
 
Mke wa Hosea na watoto wake
Mwenyezi Mungu alipoanza kuzungumza kupitia Hosea, Mwenyezi Mungu alimwambia, “Nenda ukajitwalie mwanamke wa uzinzi na watoto wa uzinzi, kwa sababu nchi ina hatia ya uzinzi wa kupindukia kwa kumwacha Mwenyezi Mungu.” Kwa hiyo alimwoa Gomeri binti Diblaimu, naye akachukua mimba na kumzalia Hosea mwana.
Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Hosea, “Mwite jina Yezreeli*maana yake Mwenyezi Mungu hupanda, kwa kuwa kitambo kidogo nitaiadhibu nyumba ya Yehu kwa ajili ya mauaji ya kule Yezreeli, nami nitaukomesha ufalme wa Israeli. Katika siku ile nitavunja upinde wa Israeli katika Bonde la Yezreeli.”
Gomeri akachukua tena mimba akamzaa binti. Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Hosea, “Mwite Lo-Ruhamamaana yake Sio mpendwa wangu, kwa maana sitaonesha tena upendo kwa nyumba ya Israeli, kwamba nisije kabisa nikawasamehe. Hata hivyo nitaonesha upendo kwa nyumba ya Yuda, nami nitawaokoa si kwa upinde, upanga au vita, wala kwa farasi na wapanda farasi, bali kupitia Mwenyezi Mungu, Mungu wao.”
Baada ya Gomeri kumwachisha Lo-Ruhama kunyonya, Gomeri alipata mwana mwingine. Kisha Mwenyezi Mungu akasema, “Mwite Lo-Amimaana yake Sio watu wangu kwa maana ninyi si watu wangu, nami si Mungu wenu.
10 “Hata hivyo Waisraeli watakuwa kama mchanga kando ya bahari, ambao hauwezi kupimika wala kuhesabiwa. Mahali pale walipoambiwa, ‘Ninyi si watu wangu,’ wao wataitwa ‘wana wa Mungu aliye hai’. 11 Watu wa Yuda na watu wa Israeli wataunganishwa tena, nao watamchagua kiongozi mmoja nao watakwea watoke katika nchi, kwa kuwa siku ya Yezreeli itakuwa kuu sana.

*1:4 maana yake Mwenyezi Mungu hupanda

1:6 maana yake Sio mpendwa wangu

1:9 maana yake Sio watu wangu