43
Yeremia apelekwa Misri
Yeremia alipomaliza kuwaambia watu maneno yote ya Mwenyezi Mungu, Mungu wao, yaani kila kitu Mwenyezi Mungu alichokuwa amemtuma kuwaambia, Azaria mwana wa Hoshaya, na Yohanani mwana wa Karea, na watu wote wenye kiburi wakamwambia Yeremia, “Wewe unasema uongo! Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, hajakutuma kusema, ‘Kamwe msiende Misri kukaa huko.’ Lakini Baruku mwana wa Neria anakuchochea dhidi yetu ili ututie mikononi mwa Wakaldayo, ili watuue au watuchukue uhamishoni Babeli.”
Basi Yohanani mwana wa Karea, na maafisa wote wa jeshi, na watu wote wakakataa kutii amri ya Mwenyezi Mungu ya kukaa katika nchi ya Yuda. Badala yake, Yohanani mwana wa Karea na maafisa wote wa jeshi wakawaongoza mabaki yote ya Yuda waliokuwa wamerudi kuishi katika nchi ya Yuda kutoka mataifa yote ambayo walikuwa wametawanywa. Pia wakawaongoza wanaume wote, wanawake na watoto, na binti za mfalme ambao Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi wa mfalme alikuwa amewaacha na Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani, na nabii Yeremia, na Baruku mwana wa Neria. Kwa hiyo wakaingia Misri kwa kutokumtii Mwenyezi Mungu, wakaenda hadi Tapanesi.
Huko Tapanesi neno la Mwenyezi Mungu likamjia Yeremia kusema: “Wayahudi wakiwa wanaona, chukua baadhi ya mawe makubwa na kuyazika katika udongo wa mfinyanzi katika njia iliyojengwa kwa matofali katika lango la jumba la kifalme la Farao huko Tapanesi. 10 Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: Nitamtumania mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli, nami nitakiweka kiti chake cha utawala juu ya haya mawe niliyoyazika hapa, naye atatandaza hema lake la ufalme juu yake. 11 Atakuja na kuishambulia Misri; atawaua waliokusudiwa kuuawa, atawateka waliokusudiwa kutekwa, na atawaua kwa upanga waliokusudiwa kuuawa kwa upanga. 12 Atachoma moto mahekalu ya miungu ya Misri, atachoma mahekalu yao na kuteka miungu yao. Kama mchungaji ajizungushiavyo vazi lake, ndivyo atakavyojizungushia Misri na kuondoka mahali hapo kwa amani. 13 Huko, ndani ya hekalu la jua*yaani Heliopoli (Mji wa Jua) nchini Misri, atabomoa nguzo za ibada, na kuteketeza kwa moto mahekalu ya miungu ya Misri.’ ”

*43:13 yaani Heliopoli (Mji wa Jua)