7
Baada ya ukuta kukamilika kujengwa upya na nikaweka milango, mabawabu wa lango, waimbaji, na Walawi waliteuliwa. Nikamweka Hanani ndugu yangu kuwa kiongozi wa Yerusalemu, pamoja na Hanania jemadari wa ngome, kwa kuwa alikuwa mtu mwadilifu na mwenye kumcha Mungu kuliko watu wengine. Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe hadi jua litakapokuwa limepanda. Walinzi wa malango wakiwa bado kwenye zamu, waamuru wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake, na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.”
Orodha ya watu waliorudi kutoka uhamishoni
(Ezra 2:1-70)
Mji ulikuwa mkubwa, tena wenye nafasi nyingi, lakini walikuwepo watu wachache ndani yake, nazo nyumba zilikuwa bado ni magofu. Hivyo Mungu wangu akaweka moyoni mwangu kuwakusanya wakuu, maafisa na watu kwa ajili ya kuorodheshwa kulingana na jamaa zao. Nilikuta orodha ya vizazi ya wale waliokuwa wa kwanza kurudi toka utumwani. Haya ndio niliyokuta yameandikwa humo:
 
Hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Azaria, Raamia, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispereti, Bigwai, Nehumu na Baana):
 
Orodha ya wanaume wa Israeli ilikuwa:
wazao wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili (2,172);
wazao wa Shefatia, mia tatu sabini na wawili (372);
10 wazao wa Ara, mia sita hamsini na wawili (652);
11 wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu), elfu mbili mia nane na kumi na nane (2,818);
12 wazao wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne (1,254);
13 wazao wa Zatu, mia nane arobaini na watano (845);
14 wazao wa Zakai, mia saba na sitini (760);
15 wazao wa Binui, mia sita ishirini na wanne (648);
16 wazao wa Bebai, mia sita ishirini na nane (628);
17 wazao wa Azgadi, elfu mbili mia tatu ishirini na wawili (2,322);
18 wazao wa Adonikamu, mia sita sitini na saba (667);
19 wazao wa Bigwai, elfu mbili na sitini na saba (2,067);
20 wazao wa Adini, mia sita hamsini na watano (655);
21 wazao wa Ateri (kupitia Hezekia), tisini na nane (98);
22 wazao wa Hashumu, mia tatu ishirini na nane (328);
23 wazao wa Besai, mia tatu ishirini na wanne (324);
24 wazao wa Harifu, mia moja na kumi na wawili (112);
25 wazao wa Gibeoni, tisini na watano (95);
26 watu wa Bethlehemu na Netofa, mia moja na themanini na nane (188);
27 watu wa Anathothi, mia moja ishirini na nane (128);
28 watu wa Beth-Azmawethi, arobaini na wawili (42);
29 watu wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi, mia saba arobaini na watatu (743);
30 watu wa Rama na Geba, mia sita ishirini na mmoja (621);
31 watu wa Mikmashi, mia moja ishirini na wawili (122);
32 watu wa Betheli na Ai, mia moja ishirini na watatu (123);
33 watu wa Nebo, hamsini na wawili (52);
34 wazao wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne (1,254);
35 wazao wa Harimu, mia tatu na ishirini (320);
36 wazao wa Yeriko, mia tatu arobaini na watano (345);
37 wazao wa Lodi, Hadidi na Ono, mia saba ishirini na mmoja (721);
38 wazao wa Senaa, elfu tatu mia tisa na thelathini (3,930).
 
39 Makuhani:
wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua), mia tisa sabini na watatu (973);
40 wazao wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili (1,052);
41 wazao wa Pashuri, elfu moja mia mbili arobaini na saba (1,247);
42 wazao wa Harimu, elfu moja na kumi na saba (1,017).
 
43 Walawi:
wazao wa Yeshua (kupitia Kadmieli kupitia jamaa ya Hodavia), sabini na wanne (74).
 
44 Waimbaji:
wazao wa Asafu, mia moja arobaini na nane (148).
 
45 Mabawabu wa malango:
wazao wa Shalumu, Ateri, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai, mia moja thelathini na nane (138).
 
46 Watumishi wa Hekalu*yaani Wanethini (pia 7:60, 73).:
wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,
47 wazao wa Kerosi, Sia, Padoni,
48 wazao wa Lebana, Hagaba, Shalmai,
49 wazao wa Hanani, Gideli, Gahari,
50 wazao wa Reaya, Resini, Nekoda,
51 wazao wa Gazamu, Uza, Pasea,
52 wazao wa Besai, Meunimu, Nefusimu,
53 wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,
54 wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,
55 wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,
56 wazao wa Nesia na Hatifa.
 
57 Wazao wa watumishi wa Sulemani:
wazao wa
Sotai, Soferethi, Perida,
58 Yaala, Darkoni, Gideli,
59 Shefatia, Hatili,
Pokereth-Hasebaimu na Amoni.
60 Watumishi wa Hekalu, na wazao wa watumishi wa Sulemani, mia tatu tisini na wawili (392).
 
61 Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:
62 wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda, mia sita arobaini na wawili (642).
 
63 Kutoka miongoni mwa makuhani:
wazao wa Hobaya, wa Hakosi na wa Barzilai (mtu aliyemwoa binti Barzilai Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).
64 Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa ukuhani, kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. 65 Kwa hiyo, mtawalaau Tirshatha: jina la heshima aliloitwa mtawala wa Yuda chini ya Ufalme wa Uajemi (pia 7:70). aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.
 
66 Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa elfu arobaini na mbili, mia tatu na sitini (42,360); 67 tena zaidi ya hao walikuwa na watumishi wa kiume na wa kike elfu saba, mia tatu na thelathini na saba (7,337); pia walikuwa na waimbaji wanaume na wanawake mia mbili arobaini na watano (245). 68 Walikuwa na farasi mia saba thelathini na sita (736), nyumbu mia mbili arobaini na watano (245), 69 ngamia mia nne thelathini na watano (435) na punda elfu sita, mia saba na ishirini (6,720).
 
70 Baadhi ya viongozi wa jamaa walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala alikabidhi kwenye hazina darkoni elfu moja§Darkoni 1,000 za dhahabu ni sawa na uzito wa kilo 8.6. za dhahabu, mabakuli hamsini, na mavazi mia tano na thelathini ya makuhani. 71 Baadhi ya viongozi wa jamaa walikabidhi kwenye hazina darkoni elfu ishirini*Darkoni 20,000 ni sawa na kilo 172. za dhahabu, na mane elfu mbili na mia mbiliMane 2,200 ni sawa na kilo 1,300. za fedha kwa ajili ya kazi hiyo.
72 Jumla ya matoleo ya watu wengine yalikuwa ni darkoni elfu ishirini za dhahabu, mane elfu mbili za fedha, na mavazi sitini na saba ya makuhani.
73 Makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji na watumishi wa Hekalu, pamoja na baadhi ya watu wengine na Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao wenyewe.
Ezra asoma Torati
Ilipotimia miezi saba, nao Waisraeli wakiwa tayari wanaishi katika miji yao,

*7:46 yaani Wanethini (pia 7:60, 73).

7:65 au Tirshatha: jina la heshima aliloitwa mtawala wa Yuda chini ya Ufalme wa Uajemi (pia 7:70).

7:65 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.

§7:70 Darkoni 1,000 za dhahabu ni sawa na uzito wa kilo 8.6.

*7:71 Darkoni 20,000 ni sawa na kilo 172.

7:71 Mane 2,200 ni sawa na kilo 1,300.