Zaburi 87
Sifa za Yerusalemu 
 Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo. 
  1 Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;   
 2 Mwenyezi Mungu anayapenda malango ya Sayuni  
kuliko makao yote ya Yakobo.   
 3 Mambo matukufu yanasemwa juu yako,  
ee mji wa Mungu:   
 4 “Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu*jina la ushairi la Misri na Babeli  
miongoni mwa wale wanaonikubali mimi:  
Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi,  
nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”   
 5 Kuhusu Sayuni itasemwa hivi,  
“Huyu na yule walizaliwa humo,  
naye Aliye Juu Sana mwenyewe  
atamwimarisha.”   
 6 Mwenyezi Mungu ataandika katika orodha ya mataifa:  
“Huyu alizaliwa Sayuni.”   
 7 Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba,  
“Chemchemi zangu zote ziko kwako.”