1 Mambo ya Nyakati
1
Adamu, Sethi, Enoshi, Kenani, Mahalaleli, Yaredi, Henoko, Methusela, Lameki. Wana wa Nuhu walikuwa ni Shemu, Hamu, na Yafethi. Wana wa Yafethi walikuwa ni Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki, na Tirasi. Wana wa Gomeri walikuwa Ashkenazi, Rifathi na Togama. Wana wa Yavani walikuwa ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani. Wana wa Hamu walikuwa ni Kushi, Misri, Putu, na Kanaani. Wana wa Kushi walikuwa ni Seba, Havila, Sabta, Raama, na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa ni Sheba na Dedani. 10 Kushi akawa baba wa Nimrodi, aliyekuwa shujaa wa Kwanza katika dunia. 11 Misri akawa babu wa Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, 12 Wapathrusi, Wakasluhi (Wafilisti walipotoka), na Wakaftori. 13 Kanaani akawa baba wa Sidoni, mwanae wa kwanza, na wa Hethi. 14 Pia akawa babu wa Myebusi, Mwamori, Mgirgashi, 15 Mhivi, Mwarki, Msini, 16 Mwarvadi, Msemari, na Mhamathi. 17 Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi, Aramu, Usi, Huli, Getheri, na Mashi. 18 Arfaksadi akawa baba wa Sala, na Sala akawa baba wa Eberi. 19 Eberi alikuwa na wana wawili wa kiume. Jina la wa kwanza lilikuwa Pelegi, kwa kuwa katika siku zake dunia ilikuwa imegawanyika. Jina la kaka yake lilikuwa Yoktani. 20 Yoktani akawa baba wa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, 21 Hadoramu, Uzali, Dikla, 22 Obali, Abimaeli, Sheba, 23 Ofiri, Havila, na Yobabu; wote hawa walikuwa uzao wa Yoktani. 24 Shemu, Arfaksadi, Sala, 25 Eberi, Pelegi, Reu, 26 Serugi, Nahori, Tera, 27 Abramu, aliye kuwa Ibrahimu. 28 Wana wa Ibrahimu walikuwa Isaka na Ishmaeli. 29 Hawa ndio wanao: mzaliwa wa kwanza alikuwa ni Nebayothi, kisha Kedari, Abdeeli, Mibsamu, 30 Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema, 31 Yeturi, Nafishi, na Kedama. Hawa ndio wana wa Ishamaeli. 32 Wana wa Ketura, suria wa Ibrahimu, walikuwa Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki, na Shua. Wana wa Yokshani walikuwa Sheba na Dedani. 33 Wana wa Midiani walikuwa Efa, Eferi, Hanoki, Abida, na Eldaa. Wote hawa walikuwa uzaowa Ketura. 34 Ibrahimu akawa baba wa Isaka. Wana wa Isaka walikuwa Esau na Israeli. 35 Wana wa Esau walikuwa ni Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu, na Kora. 36 Wana wa Elifazi walikuwa ni Temani, Omari, Sefo, Gatamu, Kenazi, Timna, na Amaleki. 37 Wana wa Reueli walikuwa ni Nahathi, Zera, Shama, na Miza. 38 Wana wa Seiri walikuwa ni Lotani, Shobali, Sebioni, Ana, Dishoni, Eseri, na Dishani. 39 Wana wa Lotani walikuwa ni Hori na Hemamu, na Timna alikuwa dada yake Lotani. 40 Wana wa Shobali walikuwa ni Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo, na Onamu. Wana wa Sebeoni walikuwa ni Aya na Ana. 41 Mwana wa Ana alikuwa ni Dishoni. Wana wa Dishoni walikuwa Hemdani, Eshbani, Ithrani, na Kerani. 42 Wana wa Eseri walikuwa Bilhani, Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani walikuwa Usi na Arani. 43 Hawa ndio wafalme walio tawala katika nchi ya Edomu kabla ya mfalme yeyote kuwatawala Waisraeli: Bela mwana wa Beori; na jina la mji wake ulikuwa Dinhaba. 44 Bela alipo kufa, Yohabu mwana wa Zera wa Bosra akatawala badala yake. 45 Yohabu alipo kufa, Hushamu wa nchi ya Watemani akatawala badala yake. 46 Hushamu alipo kufa, Hadadi mwana wa Bedadi, aliye washinda Wamidiani katika uwanja wa Moabu, akatawa badala yake. Jina la mji wake ulikuwa Avithi. 47 Hadadi alipo kufa, Samla wa Masreka akatawala badala yake. 48 Samla alipo kufa, Shauli wa Rehobothi Hanahari akatawala badala yake. 49 Shauli alipo kufa, Baal-Hanani mwana wa Akbori akatawala badala yake. 50 Baal-Hanani mwana wa Akbori alipo kufa, Hadari akatawala badala yake. Jina la mji wake ni Pau. Jina la mke wake lilikuwa ni Mehetabeli binti wa Matredi binti wa Mezahabu. 51 Hadadi akafa. Wajumbe wa ukoo wa Edomu walikuwa Timna, Alva, Yethethi, 52 Oholibama, Ela, Pinoni, 53 Kenazi, Temani, Mibsari, 54 Magdieli, na Iramu. Hawa ndio walikuwa wajumbe wa ukoo wa Edomu.