8
1 Katika mwaka wa tatu wa utawala wa mfalme Belshaza, mimi Danieli niliona maono (baada ya maono ya awali yaliyonipata). 2 Nilipokuwa nikiangalia katika ndoto, niliona kwamba nilikuwa katika mji wa Shushani wenye ngome katika jimbo la Elamu. Niliona katika ndoto kuwa nilikuwa karibu na mfereji wa Ulai. 3 Nilitazama juu na nikaona mbele yangu kondoo dume lenye mapembe mawili, limesimama pembeni mwa mfereji. Pembe moja lilikuwa refu kuliko jingine, lakini pembe ndefu ilikuwa inakua pole pole kuliko ile fupi na pembe fupi ilirefuka na kuizidi nyingine. 4 Niliona kondoo mme akiishambulia magharibi, kisha kaskazini, na baadaye kusini; hakuna mnyama mwingine aliyeweza kusimama mbele yake. Hakuna yeyote aliyeweza kumwokoa yeyote katika mkono wake. Alifanya chochote kile alichokitaka, na alikuwa mtu mkubwa sana. 5 Na nilipokuwa natafakari juu ya haya, niliona beberu akitoka magharibi, na kuvuka katika uso wa dunia yote, akikimbia kwa kasi kana kwamba hakuonekana kama aligusa ardhini. Mbuzi huyo alikuwa na pembe kubwa katikati ya macho yake. 6 Alienda mpaka kwa kondoo aliyekuwa na pembe mbili, nilikuwa nimemwona kondoo dume amesimama katika ukingo wa mfereji na mbuzi alikimbia kumwelekea kondoo dume kwa hasira kali. 7 Niliiona mbuzi ikija karibu na kondoo. Mbuzi alikuwa na hasira na kondoo, alimpiga kondoo na alizivunja pembe zake mbili. Kondoo hakuwa na nguvu za kusimama mbele zake. Mbuzi alimgonga kondoo akaanguka chini na akamkanyaga. Hapakuwa na yeyote wa kumwokoa kutoka katika nguvu zake. 8 Ndipo mbuzi alikua akawa mkubwa, lakini alipokuwa na nguvu, pembe kubwa ilivunjwa, na katika sehemu yake zilichipuka na kukua pembe nne kubwa zilizochomoza kuelekea pepo nne za mbingu. 9 Kutoka katika pembe moja ilichipuka pembe nyingine, ilikuwa ndogo hapo awali, lakini baadaye ilikuwa pembe kubwa upande wa kusini, na mashariki, na katika nchi ya uzuri. 10 Pembe ilikuwa kubwa na matokeo yake iliinua vita dhidi ya jeshi la mbinguni. Baadhi ya jeshi na nyota kadhaa zilitupwa chini duniani, na zilikanyagwa. 11 Alizidi kuwa mkubwa, mkubwa kama kamanda wa jeshi la kimungu. Sadaka za kuteketezwa za kila siku ziliondolewa mbali na yeye, na sehemu yake takatifu zilitiwa unajisi. 12 Kwasababu ya uasi, pembe ya mbuzi ilipewa jeshi, na sadaka za kuteketezwa zitasitishwa. Pembe itautupa ukweli chini ardhini, na itafanikiwa katika kila jambo ilifanyalo. 13 Kisha nilimsikia mtakatifu mmoja akiongea na mtakatifu mwingine akamjibu, “ Mambo haya yatadumu kwa muda gani, maono haya ya sadaka ya kuteketezwa, dhambi ile iletayo uharibifu, ukabidhiajia wa sehemu takatifu, na jeshi la mbinguni kukanyagwa? 14 Aliniambia, “ Itadumu kwa jioni na asubuhi zipatazo 2, 300. Baada ya hapo, mahali patakatifu patawekwa sawa.” 15 Wakati mimi Danieli, nilipoona maono, nilijaribu kuyaelewa. na hapo mbele yangu alisimama yule aliyeoneakana kama mtu. 16 Niliisikia sauti ya mtu ikiita katikati ya kingo za mfereji wa Ulai. Alisema, “Gabrieli, msaidie mtu huyu kuelewa maono.” 17 Basi alikuja karibu na mahali niliposimama. Na alipokuja, niliogopa na nilisujudia hadi chini. Aliniambia,”Fahamu, mwana wa mtu, kwamba maono ni kwa ajili ya wakati wa mwisho.” 18 Alipokuwa anaongea na mimi, nilipata usiingizi mzito nikiwa nimelala kifudifudi. Kisha alinishika na kunisimamisha. 19 Akaniambia, “Tazama, nitakuonyesha kile kitachotokea baadaye katika kipindi cha ghadhabu, kwasababu maono haya yanahusu wakati wa mwisho uliopangwa. 20 Na kuhusu kondoo mme uliyemwona, yule mwenye pembe mbili - ni wafalme wawili wa Umedi na Uajemi. 21 Mbuzi dume ni mfalme wa Ugiriki. Pembe kubwa katikati ya macho yake ni mfalme wa kwanza. 22 Na kuhusu pembe iliyovunjika, ambayo katika nafasi yake pembe zingine nne zilichipuka - hizi ni falme nne zitakazoinuka kutoka katika taifa lake, lakini hazitakuwa na nguvu kubwa. 23 Katika siku zijazo za falme hizo, wakati ambapo wahalifu watakuwa wamefikia kikomo chao, mfalme mwenye uso katili, na yeye mwenye akili sana, atainuka. 24 Nguvu zake zitakuwa kubwa, lakini si kwa nguvu zake mwenyewe. Atakuwa wa kustaajabisha kwa kile atakachokuwa anakiharibu; atafanya na kufanikiwa. Atawaangamiza watu wenye nguvu, watu miongoni wa watakatifu. 25 Ataufanya udanganyifu usitawi chini ya mkono wake kwasababu ya ujanja wake. Atawaangamiza watu wengi bila kutegemea. Atainuka pia hata kinyume cha Mfalme wa wafalme, na atavunjwa, lakini si kwa mkono wowote wa binadamu. 26 Maono kuhusu jioni na asubuhi ulizoambiwa ni ya kweli. Lakini uyafunge maono haya, kwa kuwa yanahusu siku nyingi za wakati ujao. 27 Ndipo mimi, Danieli nilichoka sana na nikalala nikiwa dhaifu kwa siku kadhaa. Kisha nikainuka na nikaenda kufanya kazi za mfalme. Lakini nilikuwa nimetishwa sana na maono, na hapakuwa na mtu yeyote aliyeweza kuyaelewa.