Mambo ya Walawi
1
Mungu alimwita Musa na alisema naye kutoka kweye hema la kukutania, akasema, “Sema na wana wa Israeli na uwaambie, 'Mwanaume yeyote miongoni mwenu akileta sadaka kwa Bwana, aleta kama matoleo katika wanyama wako, iwapo mifugo au katika kundi.” Kama matoleo yake ni ya sadaka ya kutekezwa kutoka katika kundi, atatoa dume asiyekuwa na kasoro. Atamtoa katika mlango wa kuingilia katika hema ya kukutania, ili iwe imekubaliwa mbele za Bwana. Ataweka mikono yake kichwani pa sadaka ya kuteketezwa, na ndipo itakuwa imekubaliwa badala yake kufanya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe. Ndipo atapaswa kuchinja ng'ombe mbele ya Bwana. Watoto wa Aroni, makuhani wataleta damu na kuinyunyizia katika madhabahu iliyo katika mlango wa kuingilia katika hema la kukutania. Ndipo ataichuna sadaka ya kuteketezwa na kuikata vipande. Kisha wana wa Haruni kuhani wataweka moto katika madhabahu na kuweka kuni ili kuchochea moto. Wana wa Haruni, makuhani wataweka vipande, kichwa na mafuta, watazipanga juu ya kuni zilizoko juu ya moto ulio madhabahuni. Lakini matumbo yake na miguu lazima ataiosha kwa maji. Kisha kuhani atateketeza kila kitu kilicho juu ya madhabahu kama sadaka ya kuteketeza. Italeta harufu nzuri sana kwangu; itakuwa sadaka iliyotolewa kwa moto kwa ajili yangu. 10 Kama sadaka kwa ajili ya sadaka ya kuteketeza kutoka kundi, kondoo au mbuzi, lazima atoe dume asiye na kasoro. 11 Lazima atamchinja juu ya madhabahu iliyo katika upande wa kaskazini mbele ya Bwana. Wana wa Haruni makuhani, watanyunyiza damu kila upande wa madhabahu. 12 Kisha ataikata katika vipande, pamoja na kichwa na mafuta yake, kuhani atavipanga juu ya kuni zilizo katika moto ulio madhabahuni, 13 lakini matumbo yake na miguu yake lazima ioshwe kwa maji. Kisha kuhani atatoa yote na kuiteketeza juu ya madhabahu. Ni sadaka ya kuteketezwa, italeta harufu nzuri kwa ajili ya Bwana; itakuwa sadaka ya Bwana iliyotolewa kwa moto. 14 Kama sadaka yake kwa Bwana itakuwa ni sadaka ya kuteketezwa ni ndege, ndipo ataleta kama sadaka yake aidha ni huwa au kinda la njiwa. 15 Kuhani ataileta madhabahuni, atamnyonga kichwa chake, na kuiteketeza juu ya madhabahu. Kisha damu yake itachuruzishwa juu ya pande za madhabahu. 16 Kisha atakiondoa kibofu chake pamoja na uchafu wake, na kukiweka upande wa mashariki mwa madhabahu, katika sehemu ya majivu. 17 Kisha atapasua mabawa yake, lakini hatagawanya katika vipande viwili. Kisha Kuhani atamtekeza katika madhabahu, juu ya kuni amabazo ziko juu ya moto. Itakuwa sadaka ya kuteketezwa, na italeta harufu nzuri sana kwa Bwana; itakuwa sadaka ya Bwana iliyotolewa kwa moto.