Hesabu
1
Mungu alimwambia Musa katika hema ya kukutania walipokuwa katika jangwa la Sinai. Hii ilitokea katika siku ya kwanza ya mwezi wa pili miaka miwili baadaya Waisraeli kutoka nchi ya Misri. Mungu alisema, 'fanya sensa ya wanaume wote wa Israel kutoka kila ukoo, katika familia za baba zao. Wahesabu kwa majina, wahesabu kila mume, kila mwanamume kuanzia umri a miaka ishirini na zaidi. Uwahesabu wote wanaoweza kupigana kama askari wa Israel. Wewe na Haruni mtaandika idadi ya wanaume katika makundi ya majeshi yao. Kila mwanamume kwa kila kabila, kichwa cha ukoo, lazima atumike na wewe kama kiongozi wa kabila. Haya ndiyo majina ya viongozi ambao watapigana pamoja na wewe: Kutoka kabila la Reubeni, Elizuri mwana wa Shedeuri; kutoka kabila la Simeoni, Shelumiel mwana wa Zurishadai Kutoka kabila la Yuda, Nashoni mwana wa Aminadabu; Ktoka kabila la Isakari, Nethaneli mwana wa Zuari; kutoka kabila Zebuluni, Eliabu mwana wa Heloni 10 kutoka kabila la Efraimu mwana wa Yusufu, Elishama mwana wa Ammihudi; kutoka kabila la Manase, Gamaliel mwan wa Pedazuri; 11 kutoka kabila la Benjamini mwana wa Ysufu, Abidani mwan wa Gidion; 12 Kutoka kabila la Dan, Ahizeri mwana wa Amishadai; 13 kutoka kabila Asheri, Pagieli mwana wa Okirani; 14 kutoka kabila la Gadi, Eliasafu mwana wa Deuli; 15 na kutoka kabila la Naftali, Ahira mwana wa Enani.” 16 Hawa ndio wanaume waliochaguliwa kutoka kwa watu. Waliongoza kabila za mababu zao. Walikuwa viongozi wa koo katika Israel. 17 Musa na Haruni wakawachukua wale wanaume, waliokuwa wameandikwa kwa majina, 18 na pamoja na wanaume hao waliwakusanya wanume wote katika siku ya kwanza ya mwezi wa pili. Kisha kila mwanume wa miaka ishirini na zaidi alitambua babu zake. Alitakiwa kutaja koo na famila kutoka katika ukoo. 19 Kisha Musa akaandika hesabu yao huko katika nyika ya Sinai, Kama Mungu alivyokuwa amemwamuru kufanya. 20 Kutoka uzao wa Reubeni, mtoto wa kwanza wa Israel, yalihesabiwa majina yote ya kila mwanamume mwenye umri wa miaka ishirini na zaidi wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka hesabu ya ukoo na familia. 21 Waliwahesabu wanaume 46, 000 kutoka ukoo wa Reubeni. 22 Kutoka uzao wa Simeoni yalihesabiwa majina yote ya kila mwanamume mwenye umri wa miaka ishirini na zaidi au wenye uwezo wa kwenda vitani, kutokana na hesabu ya ukoo na familia. 23 Walihesabu wanaume 59, 300 kutoka kabila la Simeoni. 24 Kutoka uzao wa Gadi yalihesabiwa majina yote ya kila mwanamume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia. 25 Walihesabu wanaume 45, 650 kutoka kabila la Gadi. 26 Kutoka uzao wa Yuda yalihesabiwa majina yote ya wanaume wenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia. 27 walihesabiwa wanume 74, 000 kutoka kabila la Yuda. 28 Kutoka uzao wa Isakari yalihesabiwa majina yote ya kila mwanamume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia. 29 Walihesabiwa wanaume 54, 000 kutoka kabila la Isakari. 30 Kutoka uzao wa Zabuloni yalihesabiwa majina yote ya kila mwanamume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia. 31 Walihesabiwa wanume 57, 400 kutoka kabila la Zabuloni. 32 Kutoka uzao wa Efraimu mwana wa Yusufu yalihesabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia. 33 Walihesabiwa wanaume 40, 500 kutoka kabila la Efraimu. 34 Kutoka uzao wa Manase mwana wa Yusufu yaliheabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu y a ukoo na familia. 35 Walihesabiwa wanaume 32, 000 kutoka kabila la Manase. 36 Kutoka uzao wa Benjamini yalihesabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia. 37 Walihesabiwa wanaume 35, 000 kutoka kabila la Benjamini. 38 Kutoka uzao wa Dani yalihesabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na mwenye uwezo wa kwenda vitani, Kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia. 39 Walihesabiwa wanaume 62, 000 kutoka kabila la Dani. 40 Kutoka uzao wa Asheri yalihesabiwa majina yote ya kila mwanume mwenye umri wa miaka ishirini au zadi na mwenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu y a ukoo na familia. 41 Walihesabiwa wanaume 41, 500 kutoka ukoo wa Asheri. 42 Kutoka ukoo wa Naftali yalihesabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na mwenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia. 43 Walihesabiwa wanaume 53, 400 kutoka kabila la Naftari 44 Musa na Haruni waliwahesabu wanaume wote hawa, pamoja na wale wanaume kumi na wawili waliokuwa wakiongoza yale makabila kumi na mawili ya Israeli. 45 Kwa hiyo wanaume wote wa Israeli wenye umri wa miak ishirini au zaidi, wote wenye uwezo wa kwenda vitani, walihesabiwa kutoka kwenye familia zao. 46 Walihesabu wanaume 603, 550. 47 Lakini wanaume toka uzao wa Lawi hawakuhesabiwa, 48 Kwa sababu BWANA alimwambia Musa, 49 “usiwahesabu wale wa kabila la Lawi wala kuwajumuisha kwenye jumla ya watu wa Israeli. 50 Badala yake, waagize Walawi kuliangalia hema la amri za agano, na kuangalia mapambo ya hema na vyote vilivyomo. Walawi watalazimika kulibeba hema na lazima wayabebe mapambo ya hema. Lazima waliangalie hema na kuyatengeneza mazingira yake. Wataiangalia masikani na kuzitengeneza kambi zinazolizunguka. 51 Kila hema litakapotakiwa kuhamishiwa eneo jingine, Walawi ndio watakaolipeleka pale. Na kila hema litakapotakiwa kusimamishwa, Walawi ndio watakao lisimamisha. Na mgeni yeyote atakayelisogelea hema lazima auawe. 52 Wakati watu wa Israeli watakaposimamisha hema zao, kila mwanaume lazima awe karibu na bango la jeshi lake. 53 Hata hivyo Walawi lazima waweke hema zao kuizunguka hiyo masikani ya amri za agano ili kwamba hasira yangu isije ikawaka juu ya wana wa Israeli. Walawi lazima wailinde hiyo masikani ya amri za agano.” 54 Wana wa Israeli walifanya yote haya. Walifanya yote ambayo BWANA aliagiza kupitia Musa.