13
1 Tena, neno la Yahwe likanijia, kusema,
2 “Mwanadamu, tabiri dhidi ya manabii wanaotabiri katika Israeli, na uwaambie wale wanotabiri nje ya fikra zao wenyewe, 'Lisikilizeni neno la Yahwe.
3 Bwana Yahwe asema hivi: Ole wao manbii wajinga ambao wafwatao roho zao wenyewe, lakini wale wasioona kitu!
4 Israeli, manabii zako wamekuwa kama mbeha kwenye aridhi iliyoharibiwa na vita.
5 Hamkwenda kwenye nyufa katika ukuta uliozunguka nyumba ya Israeli kwa ajili ya kuukarabati, ili kupigana katika vita katika siku ya Yahwe.
6 Watu wameona uongo na kufanya utabiri wa uongo, wale wasemao, “Hivi na hivi ndvyo Yahwe asemavyo.” Yahwe hajawatuma, lakini hata hivyo wamewafanya watu kutumaini kwamba ujumbe wao utakuwa kweli.
7 Je hamkusikia maono ya uongo na kufanya utabiri wa uongo, ninyi msemao, “Hivi na hivi ndivyo Yahwe asemavyo” Wakati mimi mwenyewe sikuongea?'
8 Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi, 'Kwa sababu mmesikia maono ya uongo na kuwaambia uongo-kwa hiyo hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo dhidi yenu:
9 Mkono wangu utakuwa juu yenu ninyi manabii mliodanganya maono na wale waliofanya unabii wa uongo. Hawatakuwepo kwenye kusanyiko la watu wangu, au kuandikishwa katika kumbukumbu ya nyumba ya Israeli; hawataenda kwenye nchi ya Israeli. Kwa kuwa mtajua yakwamba mimi ni Bwana Yahwe!
10 Kwa sababu hiyo, na kwa sababu wamewaongoza watu wangu kuwapotosha na kusema, “Amani!” wakati hakuna amani, wanajenga ukuta ambao wataupaka rangi ya chokaa.'
11 Waambie wale wanaopaka chokaa ukuta, 'Utaanguka chini; kutakuwa na mvua ya kufurika, na nitaleta mvua ya mawe kuufanya uanguke chini, na upepo wa dhoruba kupuliza hata kuuvunja chini.
12 Tazama, ukuta utaanguka chini. Je wengine hawakuwaambia, “Iko wapi chokaa mliyoipaka juu yake?”
13 Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Nitaleta upepo wa dhoruba katika ghadhabu yangu, na kutakuwa na mafuriko ya mvua kwenye ghadhabu yangu! Mvua ya mawe katika ghadhabu yangu itauharibu kabisa.
14 Kwa kuwa nitaurarua chini ukuta ambao mlioufunika kwa chokaa, na nitaubomoa hata kwenye nchi na kuifunua misingi yake. Hivyo utaanguka, nanyi nyote mtaangamizwa katikati ya huo.
15 Ndivyo nitakavouangamiza kwa ghadhabu yangu ukuta na wale walioupaka chokaa. Nitawaambia, “Ukuta hautaonekana tena, wala watu wanaoupaka chokaa-
16 manabii wa Israeli wale waliotabiri kuhusu Yerusalemu na wale waliokuwa wameona amani kwa ajili yake. Lakini hakuna amani! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”
17 Hivyo wewe, mwanadamu, weka uso wako dhidi ya binti za watu wako wale wanaotabiri kwa akili zao wenyewe, na kutabiri dhidi yao.
18 Sema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Ole kwa wanawake washonao hiziri kwenye kila sehemu ya mkono wao na kutengeza vitambaa vya shela kwa ajili ya vichwa vyao kwa kila kipimo, ili kuwinda watu. Je mtawawinda watu wangu ila kuokoa maisha yenu wenyewe?
19 Ninyi mmenikufuru mbele ya watu wangu kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, kuwaua watu ambao hawakutakiwa kufa, na kuyalinda maisha ya wale ambao hawatakiwi kuendelea kuishi, kwa sababu ya uongo wenu kwa watu wangu walio wasikiliza.
20 Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Niko kinyume dhidi ya hirizi ambazo mlizozitumia kuyakamata kwa hila maisha ya watu kana kwamba wamekuwa ndege. Naam, nitazichana kutoka kwenye mikono yenu; na wale watu mlio watega kama ndege-nitawaacha waende huru.
21 Nitavichana mbali vitambaa vya shela na kuwaokoa watu wangu kutoka kwenye mikono yangu, kwa hiyo hawatategwa tena kwenye mikono yenu. Mtajua kwamba mimi ni Yahwe.
22 Kwa sababu mmeuvunja moyo wa mtu mwenye haki kwa uongo, ingawa hata mimi sikutamani kuvunjwa kwake moyo, na kwa sababu mmemtia moyo badala yake matendo ya mtu mwovu ili kwamba asitaweze kurudi kutoka kwenye njia yake kuokoa maisha yake-
23 kwa hiyo hamtayaona tena maono ya uongo au kuendelea kufanya utabiri, kwa kuwa nitawaokoa watu wangu kutoka kwenye mkono wako. Nanyi mtajua kwamba mimi ni Yahwe.'”