14
1 Baadhi ya viongozi wa Israeli wakaja kwangu na kuketi mbele yangu.
2 Ndipo neno la Yahwe likanijia, likisema,
3 “Mwanadamu, hawa watu wamchukua sanamu zao kwenye mioyo yao na kuweka pingamizi la uovu wao mbele ya nyuso zao wenyewe. Je naweza kuulizwa yote na wao?
4 Kwa hiyo watangazie hivi na waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Kila mtu wa nyumba ya Israeli achukuaye sanamu moyoni mwake, au awekeye pingamizi la uovu mbele ya uso wake, na kisha yule ajaye kwa nabii-Mimi, Yahwe, nitamjibu kulingana na sanamu zake.
5 Nitafanya hivi ili kwamba niweze kuirudisha nyumba ya Israeli katika mioyo yao ambayo ilikuwa mbali nami kwa ajili ya sanamu zao.'
6 Kwa hiyo sema kwa nyumba ya Israeli, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tubuni na rudini kutoka kwenye sanamu zenu! Rudisheni nyuma nyuso zenu kutoka kwenye kachukizo yenu yote.
7 Kwa kuwa kila mmoja kutoka kwenye nyumba ya Israeli na kila mmoja wa wageni wanaoishi katika Israeli ajitengaye nami, achukuaye sanamu zake kwenye moyo wake na kuweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake mwenyewe, na kisha yule ajaye kwa nabii kunitafuta-mimi, Yahwe, nitamjibu mimi mwenyewe.
8 Hivyo nitauweka uso wangu juu ya huyo mtu na kumfanya ishara na mithali, kwa kuwa nitamkata kutoka kati ya watu wangu, na mtajua kuwa mimi ni Yahwe.
9 Kama nabii atadanganywa na kuongea ujumbe, kisha Mimi Yahwe, nitamdanganya huyo nabii; Nitanyoosha mkono wangu na kumwangamizaku toka kati watu wangu Israeli.
10 Watabeba uovu wao wenyewe; uwovu wa nabii utakua uleule kama uovu wa yule aulizaye kutoka kwake.
11 Kwa sababu hiyo basi, nyumba ya Israeli haitaenda mbali kutoka kunifuata mimi wala kujinajisi wenyewe kupitia dhambi zao zote. Watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao-hivi ndivyo Yahwe asemavyo.”'
12 Kisha neno la Yahwe likanijia, likisema,
13 “Mwanadamu, wakati nchi itakapo asi dhidi yangu kwa kufanya dhambi ili kwamba ninyooshe mkono wangu dhidi yake na kuvunja tegemea la mkate wake, na kuleta njaa juu yake na kukata mnyama kutoka kwenye nchi;
14 kisha hata kama hawa watu watatu-Nuhu, Danieli, na Ayubu-walikuwa katikati ya nchi, wangeweza kuokoa maisha yao wenyewe kwa haki-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
15 Kama nikileta wanyama waovu kwenye nchi na kuwafanya wasizae hivyo basi itakuwa hakuna mtu asiweze kupita kwa sababu ya hao wanyama,
16 kisha hata kama watu hawa hawa watatu ndani yake-kama niishivyo, asema Bwana Yahwe-wasingeweza kuwaokoa hata watoto wao wala binti; isipokuwa maisha yao yataokoka, lakini nchi itakuwa ukiwa.
17 Au nikileta upanga juu ya hiyo nchi na kusema, 'Upanga, nenda kwenye nchi na wakate wote mtu na mnyama kutoka huo',
18 kisha hata kama hawa watu watatu watakuwa katikatai ya nchi-kama niishivyo, asema Bwana Yahwe-wasingeweza kuwaokoa japo watoto wao wala binti; ila tu maisha yao wenyewe yangeokolewa.
19 Au kama nikipeleka tauni juu ya nchi na kumwaga dhahabu yangu juu yake kwa damu, ili kuwakata mtu na mnyama,
20 kisha hata kama Nuhu, Danieli, na Ayubu wangekuwa kwenye hiyo nchi-kama niishivyo, asema Bwana Yahwe-wasingeweza kuokoa hata watoto wao au binti; maisha yao pekee yangeokoka kwa haki.
21 Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: hakika nitafanya mambo makali sana kwa kuleta adhabu zangu nne-njaa, upanga, wanyama wa porini, na tauni-juu ya Yerusalemu kuwakata wote mtu na mnyama kutoka kwake.
22 Kisha, tazama! mabaki yatasalia kwake, watakaokoka wataenda pamoja na wana na binti. Tazama! Watawatokea, na mtaona njia zao na matendo yao yakiwafariji kuhusu adhabu niliyoipeleka Yerusalemu, na kuhusu kila kitu kingine ambacho nilichopeleka juu ya nchi.
23 Waliokoka watawafariji ninyi mtakapoona njia zao na matendo yao, hivyo mtayajua haya mambo niliyoyafanya juu yake, kwamba sijayafanya bure! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”