41
1 Kisha yule mtu akanileta mahali patakatifu pa hekalu na mihimili-dhiraa sita upana pande zote.
2 Upana wa maingilio ulikuwa dhiraa kumi; ukuta kila upande dhiraa tano urefu kila upande. Kisha yule mtu akapima ukubwa wa mahali patakatifu-dhiraa arobaini upana urefu na dhiraa ishirini upana.
3 Kisha yule mtu akaenda hata mahali patakatifu sana na kuipima miimili ya matokeo-dhiraa mbili-kuta pande zote zilikuwa dhiraa saba upana.
4 Kisha akapima urefu wa vyumba-dhiraa ishirini. Upana wake-dhiraa ishirini hata mbele kwenye ukumbi wa hekalu. Kisha akanambia, “Hapa ndipo mahali patakatifu sana.”
5 Kisha yule akapima kuta za nyumba-zilikuwa dhiraa sita unene. Upana wa kila upande wa chumba kuzunguka nyumba dhiraa nne upana.
6 Kulikuwa na pande tatu za vyumba, chumba kimoja juu ya kingine, vyumba thelathini, kulikuwa na kibao kitokezacho ukutani kuzunguka ukuta wa nyumba, kusaidia pande zote za vyumba, kwa kuwa hapakuwa na msaada uliokuwa umewekwa kwenye ukuta wa nyumba.
7 Hivyo mbavu za nyumba zilipanuka na kuzunguka kwenda juu, kwa kuwa nyumba ilizunguka kwenda juu, na ngazi kuelekea juu hata sehemu ya juu, kupitia sehemu ya katikati.
8 Kisha nikaona sehemu iliyoinuka kuzunguka nyumba, msingi kwa ajili ya pande za vyumba; ikapimwa fimbo nzima urefu-dhiraa sita.
9 Upana wa ukuta wa vyumba vya pembeni kwa upande wa nje ulikuwa dhiraa tano. Kulikuwa na sehemu ya wazi kwa upande wa nje wa hivi vyumba katika patakatifu.
10 Kwa upande mwingine wa hii sehemu ya wazi kulikuwa na vyumba vya makuhani upande wa nje; hii sehemu ilikuwa na dhiraa ishirini upana kupazunguka patakatifu.
11 Kulikuwa na milango kwenye vyumba vya pembeni kutoka sehemu ya wazi nyingine-njia ya mlango moja uliokuwa upande wa kaskazini, na mwingine upande wa kusini. Upana wa hili eneo la wazi ulikuwa na dhiraa tano kupazunguka.
12 Lile jengo lililokuwa limeelekea kwenye ua upande wa magaribi dhiraa sabini upana. Ukuta wake ulipimwa dhiraa tano pande zote, na ilikuwa dhiraa tisini urefu.
13 Kisha yule mtu akapapima patakatifu-dhiraa mia moja urefu. jengo lililokuwa limetengeka, kuta zake, na kwenye ua pia palipimwa dhiraa mia moja urefu.
14 Upana wa mbele kwenye ua mbele ya patakatifu pia kulikuwa dhiraa mia moja.
15 Kisha yule mtu akapima urefu wa jengo karibu na patakatifu, kwa upande wake wa magharibi, na juu ya baraza pande zote-dhiraa mia moja. Mahali patakatifu na varanda,
16 kuta za ndani na madirisha, pamoja na madirisha madogo, na baraza za pande zote kwenye pande tatu, zilikuwa zimefungwa kwa mbao.
17 Juu ya lango la kuingilia hata patakatifu pa ndani na kuwekwa karibu na kuta kulikuwa na pazia lililokuwa limepimwa.
18 Palikuwa pamepambwa na makerubi mitende; pamoja na mitende kati ya kerubi na kerubi, na kila kerubi lilikuwa na nyuso mbili:
19 uso wa mtu aliyekuwa ameelekea mtende mmoja, na uso wa mwana simba ulitazama kuelekea mtende kwa upande mwingine. Vilifunikwa kuzunguka malango ya kuingia yote ya nyumba.
20 Kutoka chini hata juu kwenye njia ya mlango, makerubi na mtende vilifunikwa na ukuta wa nje ya nyumba.
21 Mihimili ya lango la mahali patakatifu lilikuwa mraba. Umbo lao lilikuwa kama umbo la
22 kwanza madhabahu ya mbao mbele ya mahali patakatifu, ambapo kulikuwa na dhiraa tatu kwenda juu na dhiraa urefu kwa kila upande. Pembe zake mihimili, kitako, na kiunzi kilitengenezwa kwa mbao. Kisha yule mtu akanambia, “Hii ni meza ambayo itakuwa kwa ajili ya Yahwe.”
23 Kulikuwa na milango miwili kwa ajili ya mahali patakatifu na mahali patakatifu sana.
24 Hii milango ilikuwa na bawaba mbili kila mlango paneli, paneli mbili kwa ajili ya mlango mmoja na paneli mbili kwa ajili ya mwingine.
25 Ilifunikwa-juu ya milango ya mahali patakatifu ambapo makerubi na mti wa mtende kama kuta ilipambwa, kulikuwa na paa ya mbao juu ya varanda kwa mbele.
26 Kulikuwa na madidsha madogo miti ya mitende kwenye varanda pande zote. Hivyo vilikuwa vyumba vya pembeni ya nyumba, na pia ilizielekea dari.