42
1 Kisha yule mtu akanituma kwenda ua wa nje upande wa kaskazini, akanileta kwenye vyumba mbele ya ua wa nje na ukuta wa nje kaskazini.
2 Hivyo vyumba vilikuwa dhiraa mia moja karibu na mbele yake na dhiraa hamsini upana.
3 Baadhi ya hivyo vyumba vilielekea ua wa ndani na vilikuwa na dhiraa ishirini kutoka patakatifu. Kulikuwa na vyumba vitatu vinavyolingana, na kingine juu kilichokuwa kimetazama chini kuelekea kingine vilikuwa vimefunguliwa, vilikuwa na pakutokea. Baadhi ya vyumba vilielekea nje kwenye ua wa nje.
4 Njia dhiraa kumi upana dhiraa mia moja urefu kueleikea mbele ya vyumba. Milango ya vyumba ilikuwa mbele kaskazini.
5 Lakini kumbi za juu zilikuwa ndogo, kwa ajili ya njia za kutembea zilichukua kutoka kwazo sehemu kubwa kulikuwa walivyofanya kwenye vyumba vya chini na katikati usawa wa jengo.
6 Kwa kuwa orofa tatu hapakuwa na mihimili, kama zile nyua, ambazo zilikuwa na mihimili. Hivyo usawa wa vyumba vya juu vilikuwa sawa sawa katika kipimo cha kulinganisha na vyumba vya chini na usawa wa katikakati.
7 Ukuta wa nje karibu na vyumba mbele ya ua wa nje, ua uliokuwa mbele ya vyumba. Huo ukuta ulikuwa dhiraa hamsini urefu.
8 Urefu wa vyumba vya ua wa nje ulikuwa dhiraa hamsini, na vyumba vilivyokuwa vimeelekea patakatifu vilikuwa dhiraa mia moja urefu.
9 Kulikuwa na mahali pa kuingilia kwenye vyumba vidogo zaidi kutoka upande mashariki, kuingia kutoka ua wa nje.
10 Karibu na ukuta wa ua wa nje juu ya upande wa mgaribi pa ua wa ndani, mbele ya patakatifu pa ua wa nje, pia kulikuwa na vyumba na njia ya mbele yao.
11 zilikuwa kama umbo la vyumba kwa upande wa kaskazini. Zilikuwa urefu ule ule na upana na matokeo yale yale na mipangilio na madirisha.
12 Kwa upande wa kusini kulikuwa na madirisha kwenye vyumba ambavyo vilikuwa kama yale yaliyokuwa upande wa kaskazini. Aya iliyokuwa ndani ilikuwa na mlango kwenye kichwa chake, na njia ilifunguliwa kwenye vyumba tafauti. Upande mashariki kulikuwa na malango wa njia kwenye njia mwishoni.
13 Kisha yule mtu akanambia, “Vyumba vya kaskazini na vyumba vya kusini vilivyokuwa mbele ya ua wa nje ni vyumba vitakatifu amabapo makuhani wafanyao kazi karibu sana na Yahwe waweze kula chakula kitakatifu sana. Wataweka vitu vitakatifu sana-sadaka ya chakula, sadaka ya dhambi, na sadaka ya hatia-kwa kuwa hapa ni mahali patakatifu.
14 Wakati makuhani watakapoingia hapo, wasitoke nje ya mahali patakatifu kwa ua wa nje, bila kuweka mavazi karibu mahali wahudumupo, kwa kuwa hapa ni patakatifu. Hivyo watavalia mahali pengine nguo kabla ya kwenda karibu na watu.”
15 Yule mtu akamaliza kupima ndani ya nyumba na kisha akanichukua nje ya lango lililokuwa limeelekea magharibi na kuzipima sehemu zote zilizokuwa zimepazunguka hapo.
16 Akaupima upande wa mashariki na fimbo ya kupimia-dhiraa mia tano kwa fimbo ya kupimia.
17 akaupima upande wa kaskazini-dhiraa mia tano na fimbo ya kupimia.
18 Pia akaupima upande wa kusini dhraa mia tano na fimbo ya kupimia.
19 Pia akageuka na kuupima upande wa magharibi dhiraa mia tano kwa fimbo ya kupimia,
20 Akaipima pande nne. Ilikuwa na ukuta umeizunguka ilikuwa dhiraa mia tano urefu, na dhiraa mia tano upana, kulitenganisha umbo takatifu kutoka ambapo ni pa kawada.