2
1 Kwa kuwa ninyi wenyewe mnajua, ndugu, kuwa ujio wetu kwenu haukuwa wa bure.
2 Mnajua kwamba mwanzoni tuliteseka na walitutenda kwa aibu kule Filipi, kama mujuavyo. Tulikuwa na ujasiri katika Mungu kunena injili ya Mungu hata katika taabu nyingi.
3 Kwa maana mahusia yetu hayatokani na ubaya, wala katika uchafu, wala katika hila.
4 Badala yake, kama vile tulivyokubalika na Mungu na kuaminiwa injili, ndivyo tunenavyo. Tunanena, si kwa kuwafurahisha watu, lakini kumfurahisha Mungu. Yeye pekee ndiye achunguzaye mioyo yetu.
5 Kwa maana hatukutumia maneno ya kujipendekeza wakati wote wote, kama mjuavyo, wala ukutumia maneno kama kisingizio kwa tamaa, Mungu ni shahidi wetu.
6 Wala hatukutafuta utukufu kwa watu, wala kutoka kwenu au kwa wengine. Tungeweza kudai kupendelewa kama mitume wa Kristo.
7 Badala yake tulikuwa wapole kati yenu kama mama awafarijivyo watoto wake mwenyewe.
8 Kwa njia hii tulikuwa na upendo kwenu. Tulikuwa radhi kuwashirikisha si tu injili ya Mungu bali pia na maisha yetu wenyewe. Kwa kuwa mmekuwa wapendwa wetu.
9 Kwa kuwa ndugu, mnakumbuka kazi na taabu yetu. Usiku na mchana tulikuwa tukifanya kazi kusudi tusije tukamlemea yeyote. Wakati huo, tuliwahubiria injili ya Mungu.
10 Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, ni kwa utakatifu wa namna gani, haki, na bila lawama tulivyoenenda wenyewe mbele yenu mnaoamini.
11 Vivyo hivyo, mnajua ni kwa namna gani kwa kila mmoja wenu, kama baba alivyo kwa wanawe tulivyowahimiza na kuwatia moyo. Tulishuhudia
12 kwamba mlipaswa kuenenda kama ulivyo mwito wenu kwa Mungu, aliyewaita kwenye ufalme na utukufu wake.
13 Kwa sababu hiyo twamshukuru Mungu pia kila wakati. Kwa kuwa wakati mlipo pokea kutoka kwetu ujumbe wa Mungu mliosikia, mlipokea si kama neno la wanadamu. Badala yake, mlipokea kama kweli ilivyo, neno la Mungu. Ni neno hili ambalo linalofanya kazi kati yenu mnaoamini.
14 Kwa hivyo ninyi, ndugu, muwe watu wa kuiga makanisa ya Mungu yaliyoko katika Uyahudi katika Kristo Yesu. Kwa kuwa ninyi pia mliteseka katika mambo yale yale kutoka kwa watu wenu, kama ilivyo kuwa kutoka kwa wayahudi.
15 walikuwa ni Wayahudi ndiyo waliomuua Bwana Yesu pamoja na manabii. Ni Wayahudi ambao walitufukuza tutoke nje. Hawampendezi Mungu na ni maadui kwa watu wote.
16 Walituzuia tusiseme na Mataifa ili wapate kuokolewa. Matokeo yake ni kwamba wanaendelea na dhambi zao. Mwisho ghadhabu imekuja juu yao.
17 Sisi, ndugu, tulikuwa tumetengana nanyi kwa muda mfupi, kimwili, si katika roho. Tulifanya kwa uwezo wetu na kwa shauku kuu kuona nyuso zenu.
18 Kwa kuwa tulitaka kuja kwenu, mimi Paulo, kwa mara moja na mara nyingine, lakini shetani alituzuia.
19 Kwa kuwa kujiamini kwetu ni nini kwa baadaye, au furaha, au taji ya kujivunia mbele za Bwana wetu Yesu wakati wa kuja kwake? Je si ninyi zaidi kama walivyo wengine?
20 Kwa kuwa ninyi ni utukufu na furaha yetu.