23
1 Kisha Ayubu akajibu na kusema,
2 “Hata leo malalamiko yangu ni machungu; maumivu yangu ni mazito kuliko manung'uniko yangu.
3 Ee, ningejua niwezapokumwona! Ee, kwamba ningeweza kwenda alipo!
4 Ningeweka shitaka langu mbele yake na kukijaza kinywa changu hoja.
5 Ningejua ambavyo angenijibu na kufahamu ambavyo angesema juu yangu.
6 Je angehojiana nami katika ukuu wa nguvu zake? Hapana, angenisikiliza.
7 Pale mwenye haki angehojiana nami. Kwa njia hii ningeonekana bila hatia kwa mwamzi wangu.
8 Tazama, naelekea mashariki, lakini hayupo pale, na upande wa magharibi, lakini siwezi kumwona.
9 Kaskazini, anapofanya kazi, lakini siwezi kumwona, na kusini, anapojificha hata nisimwone.
10 Lakini anaijua njia ninayoichukua; atakapokuwa amenipima, nitatoka kama dhahabu.
11 Mguu wangu umeunganishwa na hatua zake; nimezitunza njia zake na sijageuka.
12 Sijaiacha amri ya midomo yake; nimeyatii maneno ya kinywa chake.
13 Lakini yeye ni wa pekee, naniawezaye kumgeuza? Analolitaka, hulitenda.
14 Kwa maana hulitimiza agizo lake kinyume changu; anamipango mingi kwa ajili yangu; ipo mingi kama hiyo.
15 Kwa hiyo, nimetishwa mbele zake; ninapofikiri kumhusu, ninamwogopa.
16 Kwani Mungu ameudhoofisha moyo wangu; Mwenyezi amenitisha.
17 Si kwa sababu nimeondolewa na giza, wala siyo kwamba giza nene limeufunika uso wangu.