24
1 Kwa nini nyakati za kuwahukumu waovu hazikuwekwa na Mwenyezi? Kwa nini siyo wale waliowaaminifu kwa Mungu huziona siku za hukumu zikija?
2 Kuna waovu waondoao alama za mipaka; kuna waovu walichukua kundi kwa nguvu na kulifanya lao.
3 Wanawadhurumu wanyonge punda wao; wanachukua ng'ombe wa mjane kuwa dhamana.
4 Wanawaondoa wahitaji katika njia zao kwa lazima; masikini wa dunia yote wanajificha kutoka kwao.
5 Tazama, masikini hawa huenda kufanya kazi kama punda-mwitu mwituni, akitafuta chakula kwa uangalifu; pengine Araba itawapatia chakula kwa ajili ya watoto wao.
6 Masikini huvuna katika mashamba ya wengine usiku; wanakusanya zabibu kidogo kutokana na mapato ya waovu.
7 Wana lala bila kujifunika wakati wa usiku; hawana cha kujifunika wakati wa baridi.
8 Wanalowanishwa na mvua ya milimani; wanalala pembeni mwa miamba mikubwa kwani hawana makao.
9 Kuna waovu wanaowapokonya yatima katika kifua cha mama zao, na waovu wawachukuao watoto kama dhamana kutoka kwa masikini.
10 Lakini masikini wanatembea uchi; wajapokaa na njaa, wanabebea wengine chakula.
11 Masikini wanazalisha vinono ndani ya nyumba za waovu; wanakanyaga mashinikizo ya waovu, lakini wanakiu.
12 Watu wananung'unika mjini; waliojeruhiwa wanaomboleza, lakini Mungu hasikilizi maombi yao.
13 Baadhi ya waovu hawa wanaiasi nuru; hawafahamu njia zake, wala kukaa katika njia zake.
14 Muaji huinuka na nuru; huuwa masikini na waitaji; ni kama mwizi wakati wa usiku.
15 Pia, mzinifu hungoja wakati wa usiku; husema, 'Hakuna anionaye.' Hujibadilisha.
16 Waovu huingia katika nyumba gizani, lakini hujifungia wakati wa mchana; hawajari nuru.
17 Kwa kuwa asubuhi kwao wote ni kama giza totoro; wanaamani na vitisho vya giza totoro.
18 Wanapotea polepole, lakini, kama povu juu ya maji; shamba lao limelaaniwa; hakuna anayekwenda kufanya kazi katika mashamba yao ya mizabibu.
19 Kiangazi na joto huondoa barafu; ndivyo kuzimu pia kunavyowaaribu waliotenda dhambi.
20 Mama yake atamsahau; polepole funza watamuuma; hatakumbukwa tena; kwa hiyo, waovu watavunjika kama mti.
21 Mwovu anamrarua mgumba; hawatendi jema lolote kwa mjane.
22 Bado Mungu huwaondoa wenye nguvu kwa nguvu zake; huinuka na kuwadhoofisha.
23 Mungu huwaacha wajione wako salama, na wanalifurahia hilo, lakini anayaangalia maisha yao.
24 Watu hawa wanatukuzwa; bado, kitambo tu, watapotea; hakika, watashushwa; watakusanywa kama wengine wote; wataondolewa kama sehemu ya juu ya masikio ya nafaka.
25 Ikiwa sivyo, nani atanithibitisha kuwa mwongo; atakaye fanya maneno yangu kuwa si kitu?”