40
1 Yahweh aliendelea kuongea na Ayubu na kusema,
2 “Je mtu yeyote anayetaka kukosoa na ajaribu kumsahihisha Mwenye enzi? Na yeye anayehojiana na Mungu, na ajibu yeye.”
3 Ndipo Ayubu akamjibu Yahweh na kusema, “
4 Tazama, mimi si mtu muhimu; je nawezaje kukujibu? Ninauweka mkono wangu juu ya mdomo wangu.
5 Ninazungumza mara moja, na sitakujibu; hakika, mara mbili, lakini sitaendelea zaidi.”
6 Kisha Yahweh akamjibu Ayubu kutoka katika dhoruba kali na kusema,
7 “Jifunge sasa mkanda kiunoni mwako kama mwanaume, kwa kuwa nitakuuliza maswali, nawe lazima unijibu.
8 Je waweza kusema kwa hakika kwamba mimi si mwenye haki? Je utanihukumu mimi ili useme wewe ni mwenye haki?
9 Je una mkono kama wa Mungu? Je waweza kutoa kishindo kwa sauti kama yeye?
10 Jivike sasa katika utukufu na katika utu; jivalie mwenyewe heshima na enzi.
11 Sambaza ziada ya hasira yako; mtazame kila mmoja mwenye kiburi na umshushe chini.
12 Mwangalie kila mmoja mwenye kiburi na umweke chini; wakanyage chini watu waovu mahali wanaposimama.
13 Wazike ardhini pamoja; zifunge nyuso zao katika sehemu zilizositirika.
14 Ndipo pia nitakapokubali ya kwamba mkono wako wa kulia waweza kukuokoa.
15 Mwangalie sasa kiboko, ambaye niliwafanya kama nilivyokufanya wewe; anakula nyasi kama ng'ombe.
16 Ona sasa, nguvu zake ziko katika viuno vyake; nguvu zake zi katika mishipa ya tumbo lake.
17 Yeye huuondoa mkia wake kama mti wa mwerezi; mishipa ya paja lake imeunganishwa pamoja.
18 Mifupa yake ni kama ya mirija ya shaba; na miguu yake ni kama kipande cha chuma.
19 Yeye ni mkuu wa viumbe vya Mungu. Ni Mungu pekee, ambaye alimwumba, anaweza kumshinda.
20 Kwa kuwa milima humpatia chakula; hayawani wa mashambani hucheza karibu.
21 Hujilaza chini ya mimiea ya kivuli katika makao ya mianzi, na katika bwawa la matope.
22 Miti yenye vivuli humfunika katika vivuli vyake; mierebi ya kijito inamzunguka pande zote.
23 Tazama, kama mto utazigharikisha kingo zake, hatikisiki; yeye anajiamini, hata kama Mto wa Yordani unajaa hadi katika pua yake.
24 Je mtu yeyote aweza kumnasa kwa ndoano, au kuichoma pua yake kwa mtego?