41
1 Je waweza kumvua mamba kwa ndoano ya samaki? Au kumfunga taya zake kwa kamba?
2 Je waweza kuweka kamba katika pua zake, au kumtoboa taya yake kwa ndoano?
3 Je atafanya maombi mengi kwako? Je atazungumza na wewe kwa maneno laini?
4 Je atafanya agano na wewe, ili kwamba umchukue kwa ajili ya mtumishi milele?
5 Je utacheza pamoja naye kama ambavyo ungecheza na ndege? Je utamfunga kwa ajili ya mtumishi wako wa kike?
6 Je makundi ya wavuvi waweza kumfanyia biashara? Je watamgawanya ili kufanya biashara miongoni mwa wafanya biashara?
7 Je waweza kuijaza ngozi yake kwa vyusa au kichwa chake kwa mikuki ya kuvulia?
8 Weka mkono wako juu yake mara moja, nawe utaikumbuka vita na hautaendelea kufanya hivyo tena.
9 Tazama, matumaini ya kila mtu ambaye hufanya hivyo ni uongo; je si kila mmoja atatupwa chini katika nchi mbele yake?
10 Hakuna aliye mkali ambaye aweza kuthubutu kumtikisa mamba; Ni nani basi awezaye kusimama mbele yake?
11 Ni nani kwanza aliyenipa kitu chochote ili kwamba niweze kumlipa? Chochote kilicho chini ya anga ni changu.
12 Sitanyamaza kimya kuhusu miguu ya mamba, wala kuhusu jambo linalohusu nguvu zake, wala kuhusu umbo lake zuri.
13 Nani awezaye kuiondoa ngozi yake? Nani anaweza kumchoma kwa silaha mara mbili?
14 Nani awezaye kuifungua milango ya uso wake, imezungukwa na meno yake ambayo yanaogofya?
15 Mgongo wake umefanywa kwa magamba yenye mistari, yamefungwa kwa pamoja kama chapa.
16 Moja li karibu na jingine na ya kuwa hakuna hewa inaweza kupita katikati yake.
17 Yameunganishwa moja kwa jingine; yamegandamana kwa pamoja, ili kwamba hayawezi kutenganishwa.
18 Mwanga hung'ara kutoka katika kupumua kwake; macho yake ni kama kope za mapambazuko ya asubuhi.
19 Ndani ya mdomo wake hutoka miali ya mwanga, chembe za moto huruka nje.
20 Katika pua zake hutoka moshi kama chungu kinachotokota juu ya moto ambao umechochewa ili uwe na joto sana.
21 Pumzi yake huwasha mkaa na kuwa mwali; moto hutoka katika mdomo wake.
22 Katika shingo yake kuna nguvu, na kitisho hucheza mbele yake.
23 Nofu za mwili wake zimeunganishwa pamoja; ziko imara katika yeye; wala haziwezi kuondolewa.
24 Moyo wake ni mgumu kama jiwe - hakika, ni mgumu kama jiwe la chini la kusagia.
25 Na anaposimama mwenyewe, hata miungu huogopa; hurudi nyuma kwasababu ya hofu.
26 Na ikiwa atapigwa kwa upanga, hauwezi kumfanya kitu chochote, wala mkuki, wala mshale, wala aina yoyote ya silaha iliyochongoka.
27 Yeye hufikiri juu ya chuma kana kwamba ni majani makavu na hufikiri juu ya fedha kana kwamba ni ubao uliooza.
28 Mshale hauwezi akamfanya akimbie; kwake yeye mawe ya kombeo huwa kama makapi.
29 Marungu huyaangalia kama majani makavu; yeye hucheka juu ya mkuki unaovuma.
30 Sehemu zake za chini zi kama vipande vilivyochongoka vya vyungu; huacha alama zilizosambaa katika udongo kana kwamba alikuwa ni chombo cha kusagia.
31 Yeye hukifanya kilindi kichemke kama chungu cha maji ya moto; huifanya bahari kama chungu cha lihamu.
32 Yeye huifanya njia ing'are nyuma yake; mtu mmoja angedhani kilindi kuwa cheupe.
33 Hakuna cha kumlinganisha juu ya dunia, ambaye yeye alikuwa ameumbwa kuishi pasipo hofu.
34 Hukiona kila kitu chenye kiburi; yeye ni mfalme juu ya wana wote wa kiburi.”