14
1 “Usiruhusu moyo wako kuwa katika mahangaiko. Unamwamini Mungu niamini pia na mimi.
2 Katika nyumba ya Baba yangu kuna makazi mengi ya kukaa; kama isingekuwa hivyo, ningekuwa nimekuambia, kwa vile ninakwenda kukuandalia mahali kwa ajili yako.
3 Kama nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena kuwakaribisha kwangu, ili mahali nilipo pia nanyi muwepo.
4 Mnajua njia mahali ninakoenda.”
5 Tomaso alimwambia Yesu, “Bwana, hatujui mahali unakoenda; Je! Tunawezaje kuijua njia?
6 Yesu alimwambia, “ Mimi ndiye njia, kweli, na uzima; hakuna awezaye kuja kwa Baba isipokuwa kupitia kwangu.
7 Kama mngeli nijua mimi, mngalikuwa mnamjua na Baba yangu pia; kuanzia sasa na kuendelea mnamjua na mmeshamuona yeye.”
8 Philipo alimwambia Yesu, “Bwana, tuonyeshe Baba, na hivyo itakuwa imetutosha.”
9 Yesu akamwambia, “Sijakuwa pamoja nanyi kwa muda mrefu, na bado hunijui mimi, Philipo? Yeyote aliyeniona mimi amemwona Baba; Jinsi gani unasema, 'Tuonyeshe Baba'?
10 Hamuamini kuwa mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Maneno ninayoyasema kwenu sisemi kwa kusudi langu mwenyewe; badala yake, ni Baba anayeishi ndani yangu anayetenda kazi yake.
11 Niamini mimi, kwamba niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani yangu; kadhalika niamini mimi kwa sababu ya kazi zangu hasa.
12 Amini, amini, nawaambia, yeye aniaminiye, mimi kazi zile nizifanyazo, atazifanya kazi hizi pia; na atafanya hata kazi kubwa kwasababu ninakwenda kwa Baba.
13 Chochote mkiomba katika jina langu, nitafanya ili kwamba Baba aweze kutukuzwa katika Mwana.
14 Kama mkiomba kitu chochote katika jina langu, hilo nitafanya.
15 Kama mkinipenda, mtazishika amri zangu.
16 Na nitamwomba Baba, Naye atawapa Msaidizi mwingine ili kwamba aweze kuwa pamoja nanyi milele,
17 Roho wa kweli. Ulimwengu hauwezi kumpokea yeye kwa sababu haumuoni, au kumjwa yeye. hata hivyo ninyi, mnamjua yeye, kwani anakaa pamoja nayi na atakuwa ndani yenu.
18 Sitawaacha peke yenu; Nitarudi kwenu.
19 Kwa muda kitambo, ulimwengu hautaniona tena, lakini ninyi mwaniona. Kwa sababu ninaishi, nanyi mtaishi pia.
20 Katika siku hiyo mtajua kwamba mimi niko ndani ya Baba, na kwamba ninyi mko ndani yangu, na kwamba mimi niko ndani yenu.
21 Yeyote azishikaye amri zangu na kuzitenda, ndiye mmoja ambaye anipenda mimi; na ambaye anipenda mimi atapendwa na Baba yangu, na Nitampenda na nitajionyesha mimi mwenyewe kwake.”
22 Yuda (siyo Iskariote) akamwambia Yesu, “Bwana, Je! Ni nini kinatokea kwamba utajionyesha mwenyewe kwetu na siyo kwa ulimwengu?
23 Yesu alijibu akamwambia, “Kama yeyote danipendaye, atalishika neno langu. Baba yangu atampenda, na tutakuja kwake na tutafanya makao yetu pamoja naye.
24 Yeyote ambaye hanipendi mimi, hashiki maneno yangu. Neno ambalo mnasikia siyo langu bali la Baba ambaye alinituma.
25 Nimeyasema mambo haya kwenu, wakati bado ninaishi miongoni mwenu.
26 Hata hivyo, Mfariji, Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisha mambo yote na atawafanya mkumbuke yote ambayo niliyasema kwenu.
27 Amani nawapa amani yangu ninyi. Siwapi hii kama ulimwengu utoavyo. Msiifanye mioyo yenu kuwa na mahangaiko, na woga.
28 Mlisikia vile nilivyowaambia, 'Ninaenda zangu, na nitarudi kwenu.' Kama mngelinipenda mimi, mngekuwa na furaha kwa sababu ninakwenda kwa Baba, kwa kuwa Baba ni mkuu kuliko mimi.
29 Sasa nimekwisha kuwaambia kabla haijatokea ili kwamba, wakati ikitokea, mweze kuamini.
30 Sitaongea nanyi maneno mengi, kwa kuwa mkuu wa dunia hii anakuja. Yeye hana nguvu juu yangu,
31 lakini ili kwamba ulimwengu upate kujua kwamba nampenda Baba, nafanya ambacho Baba ananiagiza mimi, kama vile alivyonipa amri. Inukeni, na tutoke mahali hapa.