15
1 Mimi ni mzabibu wa huu kweli, na baba yangu ni mkulima wa mzabibu.
2 Kila tawi ndani yangu ambalo halizai tunda, na husafisha kila tawi ambalo huzaa tunda huliondoa ili kwamba liweze kuzaa zaidi.
3 Ninyi tayari mmekuwa safi kwa sababu ya ujumbe ambao nimekwisha waambia.
4 Mkae ndani yangu, na mimi ndani yenu. Kama tawi lisivyoweza kuzaa peke yake lisipo kuwa katika mzabibu, kadhalika nayi, msipo kaa ndani yangu.
5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi. Adumuye ndani yangu na mimi ndani yake, mtu huyu huzaa matunda mengi, kwa kuwa pasipo mimi hamuwezi kufanya jambo lolote.
6 Ikiwa mtu yeyote hatasalia ndani yangu, atatupwa kama tawi na kukauka; watu hukusanya matawi na kuyatupa katika moto, na kuteketea.
7 Ikiwa mtadumu ndani yangu, na kama maneno yangu yakidumu ndani yenu, ombeni lolote mtakalo, nanyi mtafanyiwa.
8 Katika hili baba yangu ametukuzwa, kwamba mnazaa matunda mengi na kwamba ni wanafunzi wangu.
9 Kama baba yangu alivyonipenda mimi, mimi pia nimewapenda ninyi; dumuni katika pendo langu.
10 Ikiwa mtashika amri zangu, mtadumu katika pendo langu kama nilivyo shika amri za baba yangu na kudumu katika pendo lake.
11 Nimesema mambo haya kwenu ili kwamba furaha yangu iwe ndani yenu na ili kwamba furaha yenu ifanyike kuwa timilifu.
12 Hii ndiyo amri yangu, kwamba mpendane ninyi kwa ninyi kama nilivyo wapenda ninyi.
13 Hakuna mtu aliye na upendo mkuu kuliko huu, kwamba ayatoe maisha yake kwa ajiliya rafiki zake.
14 Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mtafanya yale niwaagizayo.
15 Siwaiti watumwa, kwa kuwa mtumwa hajui kile afanyacho bwana wake. Nimewaita ninyi marafiki, kwa sababu nimewajulisheni mambo yote ambayo nimesikia kutoka kwa Baba.
16 Hamkunichagua mimi, bali mimi niliwachagua ninyi na kuwaweka mwende mazae matunda, na tunda lenu lipate kukaa. Hii liko hivi ili kwamba chochote muombacho kwa Baba kwa jina langu, atawapeni.
17 Mambo haya ninawaagiza, kwamba mpendane kila mtu na mwenzake.
18 Kama ulimwengu utawachukia, mjuwe kwamba ulinichukia mimi kabla haujawachukia ninyi.
19 Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda kama wa kwao; Lakini kwa sababau ninyi sio wa ulimwengu na kwa sababu niliwachagua kutoka katika ulimwengu, ni kwa ajili hii ulimwengu huwachukia.
20 Kumbukeni neno ambalo niliwaambia, 'Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake.' Ikiwa walinitesa mimi, watawateseni ninyi pia; Kama walishika neno langu, wangelishika la kwenu pia.
21 Watawatendeeni mambo haya yote kwa ajili ya jina langu kwa sababu hawamjui yule aliyenituma.
22 Kama nisingekuja na kuwaambia waambia, wasingalikuwa wamefanya dhambi; lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi yao.
23 Anichukiaye mimi humchukia Baba pia.
24 Ikiwa sijafanya kazi miongoni mwao ambayo hapana mmoja aliyeifanya, wangelikuwa hawana dhambi; lakini sasa wamefanya yote mawili wameona na wamenichukia mimi na Baba yangu.
25 Hili linatokea ili kwamba neno litimie ambalo limeandikwa katika sheria yao: 'Wananichukia mimi bila sababu.'
26 Wakati mfariji amekuja, ambaye nitamtuma kwenu kutoka kwa Baba, huyu ndiye, Roho wa kweli, ambaye anatokea kwa Baba, atanishuhudia.
27 Ninyi pia mnanishuhudia kwa sababu mmekuwa pamoja nami tangu mwanzo.