Malaki
1
1 Tamko la neno la Bwana kwa Israeki kwa mkono wa Malaki.
2 “Nilikupenda, “asema Bwana. Lakini unasema, “kwa jinsi gani ulitupenda?” Esau siyo ndugu yake Yakobo?” asema Bwana. “Na bado nampenda Yakobo,
3 lakini nimemchukia Esau. nimeifanya milima yake kuwa ukiwa, na nimepafanya urithi wake kuwa makao ya mbweha wa jangwani.”
4 Kama Edomu husema, “Tumepigwa, lakini tutarudi na kujenga palipoharibiwa; “Bwana wa Majeshi asama hivi, “Watajenga lakini nitaiangusha chini; na wanaume watawaita 'Nchi ya uovu', na 'Watu ambao ambao Mungu ana hasira nao milele.”'
5 kwa macho yenu mtaona hili, na mtasema, “Bwana ni mkuu mbele ya mipaka ya Israel.”
6 mtoto amtiibaba yake, na mtumwa amtii bwana wake. ikiwa mimi, ni baba, iko wapi heshima yangu? na kama mimi ni bwana, iko wapi heshima yangu? Bwana wa majeshi asema hivi kwenu, makuhani, mnaodharau jina langu. lakini mnasema, 'tumeridharauje jina lako?
7 kwa kutoa mikate iliyonajisi madhabahuni kwangu. Na mnasema kuwa, 'Tumekuradhau kwa namna gani?' Kwa kusema hivyomeza ya Bwana imedharauliwa.
8 Mkitoa sadaka ya wanyama vipofu, hiyo siyo dhambi? na kama mkitoa vilema na wagonjwa, hiyo siyo dhambi? pelekeni hili kwa liwali; atawakubali au atainua nyuso zetu?” asema Bwana wa Majeshi.
9 Na sasa, mnajaribu kutafuta neema ya Mungu, ili kwamba awe mwema kwetu. “Na aina gani ya sadaka kwa sehemu yenu, ataziinua nyuso zenu? asema Bwana wa Majeshi.
10 Kama kungekuwa na mtu ambaye angefunga lango la Hekalu, ili kwamba kusewe na mto madhabahuni bure! lakini sina radhi na ninyi, “ asema Bwana wa majeshi, “na sitaikubali sadaka yeyote kutoka katika mikono yenu.
11 Kutoka mawio ya jua mpaka machweo jina langu litakuwa kuu katikati ya mataifa; katika kila sehemu uvumba utatolewa katika jina langu, na pia sadaka safi. Kwa sababu jina langu likuwa kuu sana katikatik ya mataif,” asema Bwana wa majeshi.
12 “lakini ninyi mnachafua mnaposema meza ya Bwana mnainajisi, na matunda yake, na chakula chake kudharauka.
13 Na ninyi pia mwasema, 'jambo hili limetuchosha, nanyi mnalidharau, “ asema Bwana wa majeshi. “Mmerudisha kilichokuwa kimechukuliwa na wanyama wa mwitu au vilema au walio wagonjwa; na ndicho mnaleta kuwa sadaka zenu! Je naweza kuikubali hii mikononi mwenu?” asema Bwana.
14 Alaniwe alye mdanganyifu, ambaye anaye mnyama dume katika kundi lake ana akaahidi kunitolea, lakini bado anatoa kwangu, mimi Bwana, ambayo ni kiujanja ujanja; kwa kuwa mimi ni mfalme mkuu,” asema Bwana wa Majeshi, “na jina langu litaogopwa katika mataifa.”