33
1 Hizi ndizo safari za wana wa Israeli hapo walipotoka katika nchi ya Misri pamoja na makundi yao ya kijeshi chini ya uongozi wa Musa na Haruni.
2 Musa aliandika maeneo yote tangu walipoondoka mpaka walipofika, kama alivyoamuriwa na BWANA. Hizi ndizo safari zao kama kutoka kwao kulivyokuwa kwa kila walipotoka.
3 Mwezi wa kwanza walisafiri kutoka Ramesi, waliondoka siku ya kumi na tano. Asubuhi siku iliyofuata baada ya Pasaka, Wana wa Israeli waliondoka wazi wazi, mbele ya machoya Wamisri wote.
4 Hii ilitokea wakati Wamisiri walipokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza, ambao BWANA alikuwa amewaua miongoni mwao, kwa kuwa pia alikuwa ameiadhibu miungu yao.
5 Wana wa Israeli walisafiri kutoka Ramesi na kuweka kambi
6 Sukothi. Walisafiri toka Sukothi na kuweka kambi Ethamu, mwisho wa nyika.
7 Wakasafiri kutoka Ethamu wakarudi mpaka Pi-Hahirothi, ambayo inaikabili Baali Zephoni, ambapo waliweka kambi kuikabili Migidoli
8 Kisha wakasafiri toka mkabala wa Pi-Hairothi na kupita katikati ya bahari kuelekea nyikani. Wakasafiri safari ya siku tatu katika nyika ya Ethamu na kuweka kambi Mara.
9 Wakasafiri kutoka Mara kufika Elimu. Pale Elimu kulikuwa na chemichemi kumi na mbili za maji na miti sabini ya mitende. hapo ndipo walipoweka kambi.
10 Walisafiri kutoka Elimu na kuweka kambi karibu na Bahari ya Shamu.
11 Walisafiri kutoka Bahari ya Shamu na kuweka kambi katika nyika ya Sini.
12 Walisafiri kutoka nyika ya Sini na kuweka kambi Dofka.
13 Wakasafiri kutoka Dofka na kuweka kambi Alushi.
14 Wakasafiri kutoka Alushi na kuweka kambi Refidimu, ambapo watu walikosa maji ya kunywa.
15 Walisafiri kutoka Refidimu na kuweka kambi kwenye nyika ya Sinai.
16 Walisafiri kutoka nyika ya Sinai na kuweka kambi Kibrothi Hataava.
17 Walisafiri kutoka Kibrothi Hataava na kuweka kambi Hazerothi.
18 Walisafiri kutoka Hazerothi na kuweka kambi Rithima.
19 Walisafiri kutoka Rithima na kuweka kambi Rimoni Perezi.
20 Walisafiri kutoka Rimoni Perezi na kuweka kambi Libna.
21 Walisafiri kutoka Libna na kuweka kambi Risa.
22 Walisafiri kutoka Risa na kuweka kambi Kehelatha.
23 Walisafiri kutoka Kehelatha na kuweka kambi kwenye Mlima Sheferi.
24 Walisafiri kutoka Mlima Sheferi na kuweka kambi Harada.
25 Walisafiri kutoka Harada na kuweka kambi Makelothi.
26 Walisafiri kutoka Makelothi na kuweka kambi Tahathi.
27 Walisafiri kutoka Ttahalathi na kuweka kambi Tera.
28 Walisafiri kutokaTera na kuweka kambi Mithika.
29 Walisafiri kutoka Mithika na kuweka kambi Hashimona.
30 Walisafiri kutoka Hashimona na kuweka kambi Moserothi.
31 Walisafiri kutoka Moserothi na kuweka kambi Bene Jaakani.
32 Walisafiri kutoka Bene Jaakani na kuweka kambi Hori Hagidigadi.
33 Walisafiri kutoka Hori Hagidigadi na kuweka kambi Jotibatha.
34 Walisafiri kutoka Jotibatha na kuweka kambi Abrona.
35 Walisafiri kutoka Abrona na kuweka kambi Ezioni Geberi.
36 Walisafiri toka Ezioini Geberi na kuweka kambi katika nyika ya Sini kule Kadeshi.
37 Walisafiri kutoka Kadeshi na kuweka kambi Mlima Hori, Pembezoni mwa nchi ya Edomu.
38 Hapo ndipo Haruni kuhani alipoenda kwenye Mlima Hori kwa amri ya BWANA na kufa kule mwaka wa arobaini bada ya Wisraeli kutoka katika nchi ya Misri, katika siku ya kwanza ya mwezi wa tano.
39 Haruni alikuwa na umri wa mika 123 alipokufa pale juu ya Mlima Hori.
40 Wakanaani, mfalme wa Aradi, ambao waliishi kusini mwa nyika katika nchi ya Kanaani, walisikia juu ya ujio wa wana wa Israeli.
41 Walisafiri kutika Mlima Hori n a kuweka kambi Zalimona.
42 Walisafiri kutoka Zalimona na kuweka kambi Punoni.
43 Walisafiri kutoka Punoni na kuweka kambi Obothi.
44 Walisafiri kutoka Obothi na kuweka kambi Abarimu, katika mpaka wa Moabu.
45 Walisafiri kutoka Abarimu na kuweka kambi Diboni Gadi.
46 Walisafiri kutoka Diboni Gadi na kuweka kambi Alimoni Diblathaimu.
47 Walisafiri kutoka Alimoni Diblathaimu na kuweka kambi kwenye milima ya Abarimu mkabala na Nebo.
48 Walisafiri kutoka mlima wa Abarimuna kuweka kambi kwenye nyanda za Moabu karibu na Yorodani huko Yeriko.
49 Waliweka kambi karibu na Yorodani, kutoka Bethi Jeshimothi mpaka Abeli Shitimu katika nyanda za Moabu.
50 Hapo BWANA alinenana Musa katika nyanda za Moabu karibu na Yorodani kule Yeriko akasema,
51 “Nena na wana wa Israeli uwaambie. 'Mtakapovuka mto Yorodani kuingia Kanaani,
52 ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote mbele yenu. Mtaziharibu sanamu zote za kuchongwa. Mtaziharibu sanamu zao za kusubu na kuharibu mahali pao pote palipoinuka.
53 Mtachukua hiyo ardhi iwe mali yenu na muishi ndani yake, kwa sababu nimewapeni hiyo nchi iwe mali yenu.
54 Mtairithi hiyo nchi kwa kupiga kura, kwa kufuata kila ukoo. Kwa zile koo kubwa kubwa mtawapa sehemu kubwa ya ardhi, na kwa zile koo ndogo ndogo mtawapa sehemu ndogo ya ardhi. Kura itakapoanguka kwenye kila ukoo, hiyo ardhi itakuwa mali yake. Mtairithi ardhi kufuata ukoo wa kabilla la jamaa zenu.
55 Lakini kama hamtawafukuza wenyeji wa nchi hiyo watoke mbele yenu, ndipo wale watu mtakaowaruhusu wakae nanyi watakapokuwa kama sindano machoni mwenu na miiba katika mbavu zenu. Watayafanya maisha yenu yawe magumu katika nchi mnayoishi.
56 Ndipo itakapotokea kuwa kile ambacho Mimi ninakusudia kufanya kwa wale watu, Nitawafanyia pia ninyi'”