34
1 BWANA akanena na Musa akasema,
2 “Waamuru watu wa Israeli na uwaambie, 'Mtakapoingia katika nchi ya Kanaani, nchi ambayo itakuwa mali yenu, nchi ya Kanaani na mipaka yake, mpaka wenu wa kusini utaendelea kutoka nyika ya Sini hadi mpaka wa Edomu.
3 Mwisho wa mpaka wa kusini utakuwa mwisho wa bahari ya chumvi kuelekea mashariki.
4 Mpaka wenu utageukia kusini kutoka mlima kuelekea Akrabimu na kupitia nyika ya Sini. na kutokea huko utaelelkea kusini mwa Kadeshi Barinea na kuelekea Hazari Adari mpaka Azimoni.
5 Kutoka huko, mpaka utageuka kutoka Azimoni kuelekea kijito cha Misri na kukifuata mpaka baharini.
6 Mpaka wa Magharibi utakuwa pwani ya bahari kuu. Huu ndio utakuwa mpaka wenuwa Magharibi.
7 Mpaka wenu wa kaskazini utaanzia kwenye bahari kuu hadi Mlima Hori,
8 kisha kutoka Mlima Hori hadi Lebo Hamathi, kisha Zedadi.
9 Mpaka utaendelea hadi Zifroni na kuishia Hazari Enani. Huu ndio utakuwa mpaka wenu wa kaskazini.
10 Kisha mtaweka alama za mpaka wenu wa mashariki ambao utaanzia Hazari Enani kuelekea kusini Shefamu.
11 Kisha mpaka wa kusini utaendelea kutoka Shefamu hadi Ribla, upande wa masharikia mwa Aini. Mpaka utaedelea upande huo wa mashariki hadi upande wa mashariki wa bahari ya Kinerethi.
12 Kisha mpaka utaendelea kuelekea kusini hadi mto Yorodani na hadi bahari ya chumvi. Hii ndiyo itakuwa nchi yenu, kwa kuifuata mipaka yake yote inayozunguka.'”
13 Kisha Musa akawaamuru watu wa Israeli akasema, “Hii ndiyo nchi ambayo mtaipokes kwa kura, ambayo BWANA ameamuru kuwapa wale makabila tisa na nusu.
14 Kabila ya uzao wa Reubeni, kwa kufuata jinsi walivyopewa urithi kwa jamaa ya kabila yao, na uzao wa kabila la Gadi, kwa kufuata jinsi walivyopewa urithi kwa jamaa ya kabila yao, na nusu ya Manase wamepata ardhi yao.
15 Wale makabila mawili na nusu wameshapata mgawo wao ng'ambo ya mto Yorodani upande wa mashariki, kuelekea kule linakotokea jua.”
16 BWANA akanena na Musa akasema,
17 “Haya ndiyo majinaya watu watakaoigawa ardhi kwa ajili ya urithi wao: Eliazari kuhani na Joshua mwana wa Nuni.
18 Mtachagua kiongozi mmoja toka kila kabila ili kuigawa ardhi kwa koo zao.
19 Haya ndiyo majina ya wanaume: Kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune.
20 Kutoka kwenye kabila la uzao wa Simeoni, Shemueli mwana wa Amihudi.
21 Kutoka kabila la Benjamini, Elidadi mwana wa Kisloni.
22 Kiongozi kutoka kabila la uzao wa Dani, Buki mwana wa Jogili.
23 Kiongozi kutoka uzao wa Yusufu, kwenye kabila la Manase, Hannieli mwana wa Efodi.
24 Kiongozi kutoka kwenye kabila la uzao wa Efraimu, Kemueli mwana wa Shiftani.
25 Kiongozi kutoka kabila la uzao wa Zabuloni, Elizafani mwana wa Parinaki.
26 Kiongozi kutoka kwenye kabila la uzao wa Isakari, Palitieli mwana wa Azzani.
27 Kiongozi kutoka kabila la uzao wa Asheri, Ahihudi mwana wa Shelomi.
28 Kiongozi kutoka kabila la uzao wa Naftali, Pedaheli mwana wa Amihudi.”
29 BWANA aliwaamuru wanaume hawa kuigawa nchi ya Kanaani na kuwapa kila kabla sehemu yao.