100
Zaburi ya shukrani.
1 Mpigieni Yahwe kelele za furaha, enyi nchi yote.
2 Mtumikieni Yahwe kwa furaha; njoni mbele zake mkiimba kwa furaha.
3 Mjue kuwa Yahwe ni Mungu; alituumba, na sisi tu wake. Tu watu wake na kondoo wa malisho yake.
4 Ingieni malangoni mwake kwa shukrani na nyuani mwake kwa kusifu. Mshukuruni yeye na litukuzeni jina lake.
5 Maana Yahwe ni mwema; uaminifu wa agano lake wadumu milele na uaminifu wake vizazi na vizazi vyote.