106
1 Msifuni Yahwe. Mshukuruni Yahwe, kwa kuwa ni mwema, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
2 Ni nani awezaye kuyahesabu mataendo makuu ya yahwe au kutangaza katika ukamilifu sifa zote za matendo yake ya kuaminika.
3 Wamebarikiwa wale watendao yaliyo mema na matendo yao yaliyo haki siku zote.
4 Ukumbuke, Ee Yahwe, unapowaonesha watu wako neema; unisaidie unapowaokoa.
5 Ndipo nitaona mafanikio ya wateule wako, wakifurahia katika furaha ya taifa lako, na utukufu pamoja na urithi wako.
6 Tumefanya dhambi kama babu zetu, tumekosea, na kufanya uovu.
7 Baba zetu hawakuyatambua matendo yako ya ajabu katika Misri; walipuuzia matendo yako mengi ya uaminifu wa agano; waliasi penye bahari, bahari ya Shamu.
8 Hata hivyo, yeye aliwaokoa kwa ajili ya jina lake ili kwamba aweze kuzifunua nguvu zake.
9 Aliikemea Bahari ya Shamu, nayo ikakauka. Kisha akawaongoza vilindini, kana kwamba ni jangwani.
10 Aliwaokoa kutoka mkononi mwa wale waliowachukia, na aliwaokoa kutoka mkononi mwa adui.
11 Lakini maji yaliwafunika washindani wao; hakuna hata mmoja aliye okolewa.
12 Ndipo waliyaamini maneno yake, nao waliimba sifa zake.
13 Lakini walisahau haraka kile alichofanya; hawakuyasubiri maelekezo yake.
14 Walikuwa na tamaa isiyotoshelezwa jangwani, wakamjaribu Mungu nyikani.
15 Aliwapa ombi lao, lakini alituma gonjwa ambalo lilishambulia miili yao.
16 Katika kambi wakawa na wivu juu Musa na Haruni, kuhani mtakatifu wa Yahwe.
17 Nchi ilifunguka na ilimmeza Dathani na iliwafunika wafuasi wa Abiramu.
18 Moto uliwaka kati yao; moto uliwaangamiza waovu.
19 Walitengeneza ndama huko Horebu na kuabudu sanamu ya kuyeyuka.
20 Wakaubadili utukufu wa Mungu kuwa mfano wa ng'ombe alaye majani.
21 Walimsahau Mungu wokozi wao, aliyefanya mambo makuu katika Misri.
22 Alifanya matendo ya ajabu katika nchi ya Hamu na matendo makuu penye Bahari ya Shamu.
23 Mungu angetangaza uharibifu wao, kama sio Musa, mteule wake, aliingilia kati kugeuza hasira yake dhidi ya kuwaangamiza.
24 Kisha waliidharau nchi yenye matunda; hawakuiamini ahadi yake,
25 bali walilalamiaka katika mahema yao, na hawakumtii Yahwe.
26 Kwa hiyo aliinua mkono wake na kuapa kwao kuwa atawaacha wafe jangwani,
27 akitawanya uzao wao kati ya mataifa, na kuwatawanya katika nchi za kigeni.
28 Waliabudu Baal ya Poeri na walizila dhabihu zilizotolewa kwa wafu.
29 Walimkasirisha kwa matendo yao, na pigo la gonjwa baya liliwashambulia kati yao.
30 Ndipo Finehasi aliinuka kuingilia kati, na pigo likakoma.
31 Ilihesabika kwake kama tendo la haki kwa vizazi vyote hata milele.
32 Pia walimkasirisha Yahwe penye maji ya Meriba, na Musa aliteseka kwa ajili yao.
33 Walimghadhabisha Musa naye akaongea haraka.
34 Hawakuyaharibu mataifa kama Yahwe alivyowaamuru,
35 bali walichangamana na mataifa na walijifunza njia zao
36 nao waliabudu sanamu, nazo zikawa mtego kwao.
37 Waliwatoa wana wao na binti zao kwa mapepo.
38 Walimwaga damu isiyo na hatia, damu ya wana na binti zao, ambao waliwatoa kama dhabihu kwa sanamu za Kanaani, waliinajisi nchi kwa damu.
39 Walinajisiwa kwa matendo yao; katika matendo yao walikuwa kama malaya.
40 Hivyo Yahwe aliwakasilikia watu wake, akawadharau watu wake mwenyewe.
41 Akawaruhusu mataifa, na wale walio wachukia wakawatawala.
42 Maadui zao wakawaonea, wakatiishwa chini ya mamlaka yao.
43 Mara nyingi alienda kuwasaidia, lakini waliendelea kuasi nao walishushwa chini kwa dhambi zao wenyewe.
44 Hata hivyo, aliiangalia dhiki yao aliposikia kilio chao kwa ajili ya msaada.
45 Alikumbuka agano lake pamoja nao na alijirudi kwa sababu ya upendo wake thabiti.
46 Aliwafanya wote waliowateka wawahurumie.
47 Utuokoe, Ee Yahwe, Mungu wetu. Utukusanye kutoka kati ya mataifa ili kwamba tuweze kulishukuru jina lako takatifu na utukufu katika sifa zako. Yahwe,
48 Mungu wa Israeli, na asifiwe toka milele na milele. watu wote walisema, “Amen.” Msifuni Yahwe. Kitabu cha tano.