120
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.
1 Katika dhiki yangu nilimuita Yahwe, naye akanijibu.
2 Uiokoe nasfi yangu, yahwe, dhidi ya wale wadanganyao kwa midomo yao na wanenao hila kwa ndimi zao.
3 Yahwe atawaadhibu vipi, na atawafanyia kitu gani zaidi, ninyi mlio na ulimi mdanganyifu?
4 Atawaadhibu kwa mishale ya shujaa iliyo nolewa kwa makaa ya moto ya mretemu.
5 Ole wangu mimi kwa sababu ninaishi kwa muda Mesheki; huko nyuma niliishi kati ya maskani ya Kedari.
6 Kwa muda mrefu sana niliisha na wale waichukiao amani.
7 Nipo kwa ajili ya amani, lakini ninenapo, wao wako kwa ajili ya vita.