121
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.
1 Nitayainua macho yangu nitazame milimani. Msaada wangu utatoka wapi?
2 Msaada wangu unatoka kwa Yahwe, aliyezifanya mbingu na nchi.
3 Hatauacha mguu wako uteleze; yeye akulindaye hatasinzia.
4 Tazama, mlinzi wa Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi kamwe.
5 Yahwe ni mlinzi wako; Yahwe ni uvuli mkono wako wa kuume.
6 Jua halitakudhuru wakati wa mchana, wala mwezi wakati wa usiku.
7 Yahwe atakulinda na madhara yote, na ataulinda uhai wako.
8 Yahwe atakulinda katika yote ufanyayo sasa na hata milele.