129
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.
1 “Mara nyingi tangu ujana wangu wamekuwa wakinishambulia,” Israeli na iseme.
2 “Mara nyingi tangu ujana wangu wamekuwa wakinishambulia, lakini hawajanishinda.
3 Wakulima wamekuwa wakilima mgonngoni kwangu; wametengeneza matuta yao marefu.
4 Yahwe ni mwenye haki; amezikata kamba za waovu.”
5 Wote waaibishwe na kurudishwa nyuma, wale wachukiao Sayuni.
6 Na wawe kama nyasi juu ya paa ambayo hunyauka kabla hayajakua,
7 ambayo hayawezi kujaza mkono wa mvunaji wala kifua cha mfunga miganda.
8 Wale wapitao karibu wasiseme, “Baraka za Mungu na ziwe juu yako; Tunakubariki katika jina la Yahwe.”