130
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.
1 Toka ndani yangu ninakulilia, Yahwe.
2 Bwana, usikie sauti yangu; masikio yako na yasikie kwa makini kuomba kwangu kwa ajili ya huruma.
3 Kama wewe, Yahwe, ungehesabu maovu, Bwana, ni nani angesimama?
4 Lakini kwako kuna msamaha, ili uweze kuheshimiwa.
5 Ninamngoja Yahwe, nafsi yangu inasubiri, na katika neno lake ninatumainia.
6 Nafsi yangu inamngoja Bwana kuliko mlinzi aingojavyo asubuhi.
7 Israeli, umtumainie yahwe. Yahwe ni wenye huruma, na yuko tayari kusamehe.
8 Ni yeye ambaye ataikomboa istaeli dhidi ya dhambi zake zote.