134
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.
1 Njoni, mtukuzeni Yahwe, enyi nyote watumishi wa Yahwe, ninyi mnaotumika hekaluni mwa Yahwe wakati wa usiku.
2 Inueni mikono yenu patakatifu pake na mtukuzeni Yahwe.
3 Mungu na awabariki toka Sayuni, yeye aliye ziumba mbingu na nchi.