133
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu, wa Daudi.
1 Tazama, jinsi ilivyo vema na yakupendeza ndugu waishi pamoja, kwa umoja!
2 Ni kama mafuta mazuri kichwani yashukayo ndevuni. Ndevu za Haruni, na yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake.
3 Ni kama umande wa Hermoni uangukao milimani pa Sayuni. Maana huko ndiko Bwana alipoamuru baraka, naam uzima milele na milele.