136
1 Oh, mshukuruni Yahwe; kwa kuwa ni mwema, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
2 Oh, Mshukuruni Mungu wa miungu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
3 Oh, mshukuruni Bwana wa mabwana, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
4 Mshukuruni yeye ambaye peke yake hufanya maajabu makuu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
5 Yeye aliyezifanya mbingu kwa hekima zake, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
6 Mshukuruni yeye alitetandaza nchi juu ya maji, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
7 Yeye aliyefanya mianga mikubwa, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
8 Mshukuruni yeye alipaye jua kutawala mchana, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
9 Mwezi na nyota vitawale usiku, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
10 Mshukuruni yeye aliyewaua wazaliwa wa kwanza wa Misri, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
11 Akawatoa Waisraeli kati yao, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
12 Kwa mkono hodari na mkono ulio nyooshwa, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
13 Mshukuruni yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
14 Na kuwapitisha Waisraeli katikati yake, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
15 Lakini akamtupa Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
16 Mshukuruni yeye aliye waongoza watu wake jangwani, kwa maana uaminifu wa agano lake ni wa milele.
17 Yeye aliyewaua wafalme wakuu, kwa maana uaminifu wa agano lake ni wadumu milele.
18 Mshukuruni yeye aliyewaua wafalme maarufu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
19 Sihoni mfalme wa Waamori, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
20 Na Ogu, mfalme wa Bashani, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
21 Mshukuruni yeye aliyewapa nchi yao kama urithi, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
22 Urithi wa Israel mtumishi wake, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
23 Yeye aliyetukumbuka na kutusaidia katika unyonge wetu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
24 Mshukuruni yeye ambaye ametupa ushindi juu ya aui zetu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
25 Yeye awapaye chakula viumbe hai wote, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
26 Oh, mshukuruni Mungu wa mbinguni, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.